MAMA AMUUA MTOTO WAKE AMFUNGA KAMBA SHINGONI AMTUNDIKA JUU YA MWEMBE MPANDA.
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi
la Polisi Mkoani Katavi linamshikilia Sado Roket (26) mkazi wa Mnyakasi kwa kumuua
mtoto wake Nchambi Tungu (11) mkazi wa Mnyakasi kwa kumpiga kwa fimbo sehemu mbalimbali za mwili
wake.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo,Kamnda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema
kuwa tukio hilo limetokea mnamo tarehe 23.01.2016
majira ya saa 19:50 katika Kitongoji cha Mnyakasi Kijiji cha Ikuba Kata ya Ikuba
Tarafa ya Mpimbwe Wilayani Mlele Mkoani Katavi.
Kamanda
Kidavashari amesema kuwa mtuhumiwa alimpatia marehemu nguo ili azifue lakini
hakuweza kufanya hivyo na ndipo mtuhumiwa alipoamua kuchukua fimbo na kuanza
kumpiga kwa kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka kupelekea kifo
chake.
Baada
ya kutekeleza azima yake mtuhumiwa alimchukua marehemu na kumpandisha juu ya
mti wa mwembe na kumfunga kwa kamba shingoni na kumwacha akining`inia ili
ionekena kuwa marehemu alijinyonga.
Chanzo
cha tukio hili ni marehemu kushindwa kufua nguo za mama yake mzazi kisha
kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake mpaka kufariki.
Hata
hivyo Jeshi la Polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa na anatarajiwa
kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika ili kujibu tuhuma
inayomkabili.
Aidha
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mikononi kwani ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za haki za
binadamu za kuishi na ni kinyume cha maadili ya kijamii badala yake wawe mstari
wa mbele kutii na kuzingatia mwenendo wa sheria za Nchi katika masuala
mbalimbali.
Comments