WAZIRI MKUU MAJALIWA AAGANA NA BALOZI WA NAMIBIA,AKUTANA NA BALOZI WA FINLAND NCHINI.
Na.Issack
Gerald-Katavi
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia
ambaye anamaliza muda wake, Bwana Japhet Isaack.
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizungumza na balozi Namibia nchini, Mhe. Japhet Isaack ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016 |
Akizungumza
na Balozi Isaack leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri
Mkuu ameshukuru Balozi huyo na kumumwomba waendeleze uhusiano mwema
ulipo baina ya nchi hizi mbili ambao ulianza tangu enzi za
kugombania uhuru ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.
“Namibia
ni nchi yenye uchumi uanaokua haraka, na mmefanikia katika baadhi ya
sekta , hivyo ningependa Tanzania ijufunze kutoka kwenu hasa katika sekta
za Utalii, Afya, na Elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia,
alitumia fursa hiyo kuwakaribisha raia wa Namibia kuja kuwekeza
nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda na kuendeleza
maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja
na kutatua tatizo la ajira nchini.
Kwa
upande wake, Balozi Isaack amesema kwa kipindi alichokaa
Tanzania amejifunza mengi, na amefurahishwa ambavyo Waziri Mkuu pamoja
Serikali kwa ujumla inavyofanyakazi kwa kasi na kwa mafanikio makubwa.
“Hongera,
ninafurahishwa na unavyofanya kazi hongera sana”, alisema Balozi Isack.
Pia, amefurahi sana kipindi chote alichokaa Tanzania kwani kimekuwa na matukio
mengi yenye kumbukumbu nzuri kwake.
Balozi
Isack ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe ili
zishirikiane zaidi katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi.
WAKATI
HUO HUO,WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo
na Balozi wa Finland nchini, Bwana Pekka Hukka.
Mkuu,Kassim Majaliwa akisalimiana na balozi wa Finland nchini Tanzania Mhe. Pekka Hukka kabla ya mazungumzo yao ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Januari 8, 2016 |
Akizungumza
jana na Balozi Hukka,alipomtembelea ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es
salaam, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa namna ambavyo nchi ya Finland
imeendelea kuisaidia Tanzania na kumumwomba waendeleze uhusiano
mwema uliokuwepo kwa zaidi ya miaka 50 sasa.
“Ninashukuru
na kutambua mchango wa nchi yako wa kuisaidia Tanzania katika sekta
mbalimbali ikwemo Utalii na Biashara, ninashukuru sana kwa hilo”
alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia,
alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kutoka Finland kuja kuwekeza
katika sekta ya viwanda na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya
uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira
nchini.
Waziri
Mkuu, pia ameendelea kwa kusema Serikali imedhamiria kukusanya mapato
kikamilifu na kuzuia mianya ya upotevu wake, hivyo ameiomba Serikali ya Finland
isaidie katika kujenga uwezo wa namna bora zaidi ya utekelezaji wa
dhamira hiyo, kwa kuwa Finland ni kati ya nchi zenye mifumo bora na
madhubuti ya ukusanyaji wa mapato.
Kwa
upande wake, Balozi Hukka amesema nchi yake kupitia Balozi za Tanzania na
Finland zimeanza jitihada za kuandaa utaratibu kwa ajili ya kuwekeza nchini ,
na kuna baadhi ya kampuni tayari ziko nchini.
Habari hii imetolewa
na Ofisi ya mawasiliano ya Waziri Mkuu na Klutwa kwako na P5 TANZANIA,asante kwa kuwa nami.
Comments