SERIKALI YATOA MILIONI 999,376,000/= KUGHARIMIA ELIMU BURE MKOANI MWANZA
Na.Issack Gerald-Mwanza.
Serikali ya awamu
ya Tano chini ya Raisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe
Josefu Magufuri Imetoa kiasi cha shilingi milioni 999,376,000 kwa ajiri ya
kughalimia elimu kwa shule za msingi na Sekondari kwa mwezi januari.
Akizungumza juzi na wakuu wa wilaya ,
Maafisa Elimu, Na wakurugenzi mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo amesema kuwa fedha hizo zimetolewa tangu
desemba 30 mwaka jana na kuingizwa
kwenye akaunti za shule husika.
Mulongo ameeleza kuwa shule za msingi
imeingizwa Milioni 642,648,000 ambazo zimegawanywa kwenye ruzuku za shule,
fidia ya ada za wanafunzi, vyakula kwa shule za Bweni na shule za msingi kiasi
cha shilingi milioni 356,728,000 na kuwataka wakuu wa shule zote kuepuka
ubadhilifu wa aina yoyote wa fedha hizo.
Aidha Bw Mlongo amesema kuwa serikali
itaendelea kutoa fedha kila mwezi na kwamba wazazi na walezi watakao shindwa kuwapeleka watoto wao
shule watachukuliwa hatua na kuwajibishwa kisheria.
Asante
kwa kuendelea kunifuatilia kwa habari mbalimbali kupitia
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments