TUME YA ARDHI MPANDA YATOA TAARIFA YA UCHUNGUZI MIGOGORO YA ARDHI KWA BAADHI YA VIJIJI
Na.Issack Gerald-Mpanda
TUME ya uchunguzi wa migogoro ya ardhi
imetoa taarifa baada ya kufanya uchunguzi katika vijiji vya Ikaka, Nkungu na Kapalamsenga
wilayani Mpanda.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu maazimio
yaliyofikiwa baada ya kupokea taarifa hiyo, Mkuu wa wilaya ya Mpanda Bw. Paza
Mwamlima amesema miongoni mwa maazimio ni pamoja na halmashauri ya wilaya ya
Mpanda kuwa na utaratibu wa kupima ardhi katika vijiji na iwe inatoa ushauri wa
kitaalam kwenye kamati za ardhi za vijiji.
Aidha, amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya
Mpanda kupitia idara ya ardhi na maliasili afungue mashtaka, baada ya uongozi
wa kijiji cha Kapalamsenga, uliokuwepo kukiuka sheria ya wanyamapori na kuuza
eneo la Lyamgoloka kwa wananchi 52 mwaka 2013.
Maeneo hayo ni miongoni mwa maeneo mengi yenye
migogoro ya ardhi Mkoani Katavi ambapo mogogoro mingi wamekuwa wakilalamikiwa
idara ya ardhi kwa kupima kiwanja kwa zaidi ya mtu mmoja.
Comments