WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE AMPA POLE
Na.Issack Gerald
WAZIRI
MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole mke wa Baba wa
Taifa, Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia
Nyerere.
Akizungumza
na mama Maria alipomtembelea nyumbani kwake jana(Jumanne, Januari 12,2016),
Msasani jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Mama Maria
Nyerere pamoja na familia na kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu
katika kipindi hiki kigumu baada ya kuondokewa na mpendwa wao.
“Kipindi
hiki ni kigumu, hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo, pia tutajumuika
nanyi katika kipindi hichi chote, tuendelee kuwa watulivu na kumwomba Mungu”
alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Ndugu
wa marehemu, John Shibuda (aliyewahi kuwa mbunge wa CHADEMA) ameeleza kutokea
kwa msiba huo. Ambapo amesema “Desemba, 19 mwaka huu Leticia Nyerere alipelekwa
nchini Marekani kwa matibabu na alifariki dunia katika hospitali ya Doctors
Community iliyopo Lanham, Maryland juzi saa 2 usiku kwa saa za Afrika
Mashariki.
Aidha,
Shibuda amemshukuru Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kwenda kuipa pole familia
na Serikali kwa namna ambavyo inatoa ushirikiano mzuri kwa familia.
Naye,
Rose Nyerere amesema familia inaendelea na maaandalizi, hivyo watatoa taarifa
ya baada ya kuandaa utaratibu wa siku ambayo mwili utaletwa nchini, kuagwa na
hatimaye kuzikwa Butiama.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Waziri
Mkuu mstaafu Frederick Sumaye ambaye amelazwa siku kadhaa zilizopita katika
Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini
Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu Majaliwa, amesema amefarijika baada ya kumuona Waziri Mkuu huyo
mstaafu akiendelea vizuri na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kumpatia
matibabu na kumhudumia vizuri. Pamoja na kumpa pole, Waziri Mkuu
amemwombea apone haraka ili aweze kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Naye,
Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa
kumtembelea hospitalini hapo, pia ameipongeza Serikali kwa jitihada mbalimbali
inazofanya ili kusaidia wananchi na hatimaye kuiletea nchi maendeleo.
“Naipongeza
Serikali kwa namna ambavyo inaendelea kutekeleza majukumu yake katika masuala
mbalimbali yenye lengo la kusaidia wananchi” alisema Sumaye.
Waziri
Mkuu Majaliwa, pia amemtembelea na kumjulia hali Balozi Hassan kibelloh ambaye
amelazwa na anaendelea kupatiwa matibabau katika Taasisi ya Jakaya Kikwete
iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Asante kwa kuendelea
kuchagua P5 TANZANIA MEDIA
Chanzo cha Habari: Ofisi ya Waziri mkuu
Comments