BABA NA MAMA WA KAMBO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA MANYANYASO NA KUMNYIMA CHAKULA MTOTO WAO
Na.Issack Gerald-KATAVI
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani
Charles (40) Mkazi wa Kasimba anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa
kosa la kumnyanyasa mtoto wake anayeitwa Adam Ramadhani (17) ambaye ni mwanafunzi
wa shule ya Sekondari Kashaulili sambamba na kumnyima mambo mengine ya msingi
kama chakula.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda Radio, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani
Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa Jeshi la Jeshi la polisi limeshughulikia
tatizo hilo la unyanyasaji baada ya kupokea taarifa kutoka kituo cha matangazo
ya Mpanda Radio FM.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa baada ya
taarifa hiyo jeshi la polisi lilimpokea mtoto huyo kituoni na kuanza kulifatia
suala hilo ambapo mtoto huyo alieleza kuwa alikuwa anaishi na baba yake mzazi
na mama yake mlezi au wa kambo aitwaye Joyce Sino.
Kwa mjibu wa maelezo ya mtoto aliyenyanyaswa
kwa nyakati tofauti alisema kuwa manyanyaso yalianza mara baada ya mama yake
kufariki ambapo awali waliishi vizuri kabla
ya kifo cha mama yake lakini ghafla hali ilibadilika na akawa hapatiwi mahitaji
ya kimaisha yakiwemo mavazi, chakula, matibabu na mahitaji ya shule kutoka kwa
wazazi wake licha ya wazazi wake kupewa misaada kanisani na mwisho alifukuzwa
na wazazi wake tarehe 29.12.2015 kwamba asikanyage kwake tena.
Baada ya tukio hilo tarehe 31.12.2015 majira
ya asubuhi jeshi la polisi lilituma hati ya wito kwa baba mzazi wa mtoto ambaye
baada ya kuipokea alikuja kituoni na wenzake wawili kujihami kwa kufungua
taarifa ya upotevu wa tarehe 01.01.2016.
Kufuati hali hiyo,Jeshi la Polisi limefungua
jalada la uchunguzi ambapo upelelezi ulikamilika na kumfikisha mtuhumiwa Ramadhani
Charles mahakamani kwa kesi ya kushindwa kutoa mahitaji na uangalizi.
Kesi ya mtu huyu inatarajiwa kutajwa tarehe
01.02.2016. pia, jitihada zinafanyika za kumkamata Joyce Sino ili afikishwe
mahakamani kwa kosa hilo hilo.
Hata hivyo Kamanda wa polisi Mkoani Katavi
Dhahiri Kidavashari ametoa wito kwa wazazi kuacha vitendo vya unyanyasaji kabla
hatua za kisheria hazijawakabidhi.
Mkoa wa Katavi,ni miongoni mwa mikoa ambayo
ukatiri umekuwa ukitokea kwa nyakati tofauti.
Asante kwa kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Endelea kuhabarika
Comments