JAMII MWANZA YATAKIWA KUTAWANYANYAPAA WAATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA
Na.Issack Gerald-Mwanza.
Jamii
nchini imetakiwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake
iwasaidie kuondokana na matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo
vya utimamu wa akili (Sobar House).
Rai
hiyo imetolewa Bw Eddy Darkis Meneja wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To
Life Sobar House Pasiansi Manispaa ya
Ilemela Mkoani Mwanza, ambacho husaidia wahanga wa dawa za kulevya kuachana na
matumizi ya dawa hizo.
Bw
Darkis amesema kuwa badhi ya wanajamii wamekuwa wakiwanyanyapaa wahanga wa dawa
za kulevya, jambo ambalo linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa hizo
nchini ambapo wahanga zaidi ya 50 wamepatiwa tiba huku wengine 25 wakiendelea
vizuri.
Ripoti
ya Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa wa habari za kupiga vita uharifu,
biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini OJADACT Bw Edwini Soko Miezi 6
ili yopita,idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya Jijini Mwanza imefikia zaidi
ya watu elfu kumi.
Asante kwa kuendelea
kuchagua P5 TANZANIA MEDIA
Chanzo:Mwandishi
wetu Mwanza
Comments