WAZIRI MKUU AKUTANA NA MABALOZI WAWILI NCHI TOFAUTI-P5 TANZANIA MEDIA INAKUJUZA
Na.Issack
Gerald
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekuatana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili
kutoka nchi za Qatar na Kuwait.
Akizungumza
kwa nyakati tofauti na mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es
salaam, Waziri Mkuu amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia,
pamoja na namna ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi
kuendeleza ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi zao.
Kwa
upande wake,
Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim al Maadad amesema Serikali yake
itaendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua
kubwa na inaweza kutoa msaada kwa Tanzania.
Amesema
Quwait iko tayari kuwekeza nchini katika sekta ya kilimo, kwa vile ardhi
ya Tanzania ni yenye rutuba na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja
sekta nyingine ambazo wangependa kuwekeza ni pamoja na sekta ya
uvuvi na viwanda.
Naye,
Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem
ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia
‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Balozi
Najem, pia ameshauri vituo vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya
kazi kwa ushirikiano zaidi ili kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Chanzo cha Habari:Ofisi ya Waziri Mkuu
Comments