MAFURIKO YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Shule ya Msingi Nsemulwa iliyopo kata
ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,mpaka sasa imesajili Jumla ya wanafunzi 513 wa darasa la kwanza na Chekechea na hatimaye
kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa,madawati na matundu ya vyoo.
Hayo yamebainishwa na Afisa elimu
kata ya Nsemulwa Bw.Gerigori John Mshota wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio
shuleni hapo.
Amesema kati ya wanafunzi 513,wanafunzi
wa darasa la kwanza waliopo ni 318 huku
chekechea wakiwa 195 na kufikia jumla ya wanafunzi 1945 waliopo kati
shule hiyo kwa sasa ambapo kwa uwiano wa
walimu 19 waliopo,kila mwalimu anatakiwa kufundisha wanafunzi 102.
Amesema changamoto zilizopo ni
upungufu wa vyumba vya madarasa 6,madawati 504 ambapo madarasa yaliyopo kwa
sasa ni 7,mawati 200 huku matundu ya vyoo yakiwa 7.
Asubuhi ya leo,P5 TANZANIA MEDIA Na Mpanda Radio zimefika shuleni hapo na
kushuhudia mwalimu mmoja akifundisha walimu 318 sababu kubwa ikitajwa kuwa na
uhaba wa walimu.
Mwalimu Joyce Mwandega ambaye ndiye amekabidhiwa wanafunzi hao wa darasa la
kwanza katika shule ya Msingi Nsemulwa amezungumza na Mpanda Radio fm kutokana
na hali iliyopo kuhusu wingi wa wanafunzi katika shule hiyo.
Hata hivyo ameiomba serikali na wadau
wa elimu kusaidia kutatua changamoto za shule hiyo ambapo kuna uwezekano wa
wanafunzi wakafikia idadi ya zaidi ya 2000 watakaokuwa katika shule hiyo
tofauti na siku zote.
Comments