VIONGOZI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA SONAMCU MKOANI RUVUMA WASIMAMISHWA KAZI NA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA
Na.Issack Gerald-Ruvuma
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha
mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha Ushirika
cha SONAMCU.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa (Picha kwa hisani ya Ofisi ya Waziri Mkuu) |
Moja ya mashamba ya tumbaku Mkoani Ruvuma |
Akizungumza
jana katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu Ndogo
ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la tumbaku wa Wilaya ya
Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa
pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye
ni Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini.
Waziri
Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika tumbaku cha
SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika utekelezaji wa agizo la
Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda nchini.
Waziri
Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na kukagua
mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda hicho kuzimwa miaka
kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za kuendelea na uzalishaji.
Pia,
amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi. Stela
Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda hicho cha
kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi wote wa Chama Kikuu
cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma hizo na kutaka wafikishwe
Mahakamani.
“Serikali
imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji vimebaki
vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema Waziri Mkuu huku
akishangiliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wakulima wa
tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia mfumo wa Vyama vya Ushirika na
namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao hadi kushindwa
kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya mazao yao.
Aidha,
Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya Mahakama
baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao wamehusika na wizi
wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni 800 kwa kipindi cha mwaka 2011
hadi 2014 tayari wamefikishwa Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia,
amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima
hao ili kupatia ufumbuzi matatizo yao.
Aidha,
ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa linaongeza
pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa na kukua kwa uchumi
wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda na kuviendesha Vyama Vya Ushirika
kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Waziri
Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara hiyo leo,
kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na kurejea jijini Dar es
Salaam.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea
kuhabarika na P5 TANZANIA
Comments