WATATU WAUAWA WILYANI MLELE KATIKA MATUKIO MAWILI TOFAUTI,LIMO LA BABA NA MWANAWE KULIWA NYAMA NA SIMBA
Na.Issack
Gerald-Mlele Katavi
Watu watatu wamekufa katika matukio mawili
tofauti Wilayani Mlele Mkoani Katavi likiwemo tukio la baba na mwanae kuliwa na
samba jike mzee.
Baadhi ya Simba katika Hifadhi ya taifa ya wanayama ya Katavi |
Katika tukio la kwanza,akithibitisha kutokea
kwa tukio hilo,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa
tukio hilo limetokea mnamo Januari 4 mwaka huu majira ya saa ya saa 3 usiku katika
maeneo ya kitongoji cha makaburi wazi kata ya Starike Tarafa ya Nsimbo Wilayani
Mlele Mkoa wa Katavi.
Kidavashari amesema,wawili waliofahamika kwa
majina ya John Jeremiah (41) mkazi wa
Matandarani na Patrick John (05) ambaye ni mtoto wa marehemu John Jeremiah wote
kwa pamoja waliuawa kwa kushambuliwa vikali na simba jike mzee.
Kamanda Kidavashari amesema,katika tukio
hilo,simba huyo alifika katika nyumba ya marehemu ya John Jeremiah ambayo ni kambi ya muda kwa ajili ya uangalizi
wa mashamba na kuanza kushambulia kuku wawili, ambapo punde aliingia ndani ya
kaya ya marehemu John Jeremiah na kumshambulia vibaya sehemu za siri, shingoni
na kichwani ambapo licha ya kupiga kelele za kuomba msaada ziliweza kusikika
kwa majirani hakupata msaada wa haraka kuokoa maisha yake.
Baada ya hapo simba huyo alimchukua marehemu
Patrick John mpaka vichakani na kuanza kumla nyama ambapo Mpaka kufikia alfajiri ya siku ya
tukio kabla ya simba huyo kuuawa,alikuwa amembakiza marehemu kichwa na mikono.
Kuhusiana na tukio hilo,Kamanda Kidavashari amesema
Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa wanyama pori TANAPA walifanya
msako na kufanikiwa kumkuta simba huyo akiendelea kumla nyama Patrick John
ambapo hata hivyo samba huyo aliuawa.
Katika tukio la Pili,mtu mwingine
aliyefahamika kwa jina la Heleni Malelemba(40) mkazi wa kitongoji cha Uzumbura
aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni na kichwani na watu
wasiojulikana.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi
Dhahiri Kidavashari amesema kuwa tukio hilo,limetokea Januari 4 mwaka huu
majira ya saa saba usiku katika kitongoji cha Uzumbura kijiji cha Ikuba, Tarafa
ya Mpimbwe, Wilayani Mlele.
Amesema kuwa,siku ya tukio,marehemu alikuwa
anaendesha pikipiki aina ya TOYO rangi Nyekundu isiyokuwa na namba za usajili
akitokea senta ya usevya kuelekea nyumbani kwake Uzumbura, ambapo akiwa njiani
ndipo alipoviziwa na watu wasiojulikana na kufanyiwa mauaji hayo kisha
watuhimiwa kutokomea kusikojulikana pasipo kuchukua pikipiki ya marehemu.
Chanzo cha
tukio hili bado hakijafahamika na upelelezi unaendelea kwa kushirikiana na
wakazi wa eneo la Tarafa ya Mpimbwe ili kubaini sababu iliyopelekea
mauaji haya ambapo Mpaka sasa hakuna watu walioshukiwa na kukamatwa kuhusiana
na tukio hili ili sheria iweze kuchukua mkondo kwa wahusika wote.
Kufuatia matukio hayo,Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Katavi anatoa wito kwa wananchi hasa wakulima na wafugaji ambao shughuli zao
huzifanya au hutegemea porini au mazingira karibu na mbuga za wanyama,kuzingatia
usalama wao kwanza kwa kuhakikisha wanakuwa makazi imara na salama dhidi ya
wanyama wakali wa porini.Pia, anaendelea kuwaonya watu wanaopenda kujichukulia
sheria mikononi kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.
Asante kwa kuendelea
kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Comments