BREAKING NEWS : WALIMU 120 MIKOA YA RUKWA,KATAVI NA KIGOMA WAPATIWA MAFUNZO KUINU KIWANGO CHA UFAULU WA WANAFUNZI
Na.Issack
Gerald-MPANDA
JUMLA ya Walimu 120 wa Shule za msingi kutoka halmashauri 8
za Mikoa ya Rukwa, Kigoma na Katavi
wanashiriki mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu na wanafunzi katika ufundishaji
na ujifunzaji ili kuboresha taaluma na kuongeza kiwango cha Ufaulu kitaifa.
Akifungua Mafunzo hayo
katika Shule ya Sekondari Mwangaza Manispaa ya Mpanda Mgeni rasmi, Kaimu Afisa
Elimu Mkoa wa Katavi Said Mwapongo, amewataka walimu walioshiriki mafunzo
kuhakikisha wanawajengea uwezo walimu wenzao ambao hawakushiriki mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yanalenga
walimu wa masomo ya Kiswahili, kingereza na hisabati, ikiwa Sehemu ya mpango wa
Matokeo makubwa sasa (BRN), yalioandaliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, na yameanza Januari 4 na yatamalizika
Januari 8 mwaka huu.
Baadhi ya wajumbe wa
semina hiyo wamesema kuwa,walimu hao kupatiwa mafunzo hayo kutaongeza ufanisi
katika kutekeleza haraka mpango wa Mtokeo Makubwa sasa na kupunguza idadi ya
wanafunzi wanaoshinwa kufaulu mithani kwa kiwango kikubwa.
Hivi karibuni Wakati
Mkoa wa Katavi ukishika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya darasa la
saba,Mkoa jirani wa Rukwa kwa mjibu wa Mkuu wa Mkoa wa mkoa huo Magalula Said
Magalula,amesema mkoa huo umeshika nafasi ya tatu kutoka mwisho katika shule za
msingoi zilizofanya mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2015.
Endelea
kuwa na P5 TANZANIA hivi punde kwa undani wa habari hii
Comments