WAWILI AKIWEMO ASKARI WA JESHI LA POLISI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MWANZA KWA TUHUMA ZA MAUAJI
Na.Issack Gerald-Mwanza
Watu wawili akiwemo askari wa Jeshi la Polisi wanashikliwa na jehi la polisi kwa makosa ya mauaji katika
maeneo tofauti Mkoani Mwanza.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Justus Kamgisha |
Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Justus Kamugisha amesema katika tukio
la kwanza,Askari wa Jeshi la Polisi
PC F.4965 Joel Francis (41)wa kambi ya polisi Mabatini wilayani Nyamagana mkoani Mwanza anashikiliwa
na Polisi kwa tuhuma za mauaji dhidi ya Rafiki yake.
Kamanda wa Polisi Mkaoni humo SACP Justus
Kamugisha amemtaja aliyeuwawa kuwa ni Donald Magalata(30)aliyekuwa milinzi wa
Mwanza hoteli ambapo amesema,tukio hilo limetokea Januari mosi mwaka huu.
Kamanda Kamugisha ameeleza kuwa PC
Francis, januari mosi mwaka huu majira ya saa 7:00 usiku alimfunga pingu
miguuni ndani mwake na kumpiga kwa madai kuwa pochi yake iliyokuwa na vitu vyake haikuonekana na
kuhisiwa kuwa aliiba.
Hata hivyo Marehemu alijaribu kuomba
msaada kwa majirani ambapo walifika eneo la tukio na kumpeleka hospitali ya
Rufaa ya Bugando na kufariki dunia usiku wa kuamkia januari 02 mwaka huu.
Aidha
Kamanda Kamgisha ameeleza kuwa Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi na
atafikishwa mahakani pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapo kamilika.
Wakati huo huo katika tukio la pili,Kamanda
Kamgisha amesema,Mwana mme moja mkazi wa Izunge Bwiro wilayani Ukerewe mkoani
Mwanza anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji baada ya kugombania mwanamke katika ukumbi wa
disco kijijini humo.
Kamanda wa polisi mkoani Mwanza SACP
Justus Kamugisha amesema kuwa tukio hilo limetokea January 2 mwaka huu majira
ya saa 6 usiku na kumhusisha Bw Michael Charles(26) aliyemuua Ngereja Mashenene(30).
Kamanda Kamugisha ameeleza kuwa Bw
Michaele Charles alimchoma kisu kifuani Bw Ngereja baada ya kugombania mwanamke katika
ukumbi wa Disko jina lake limehifadhiwa na baadae akafariki dunia wakati
akipelekwa Hospitalini.
Aidha Mtuhumiwa amekamatwa na
upelelezi wa shauri hili utakapo kamilika atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazo mkabuili.
Comments