WAZIRI MKUU ASEMA SERIKALI HAIJARIDHIA VIWANGO VIPYA VYA NAULI YA MABASI YAENDAYO KASI
Na.Issack Gerald-Dar es Salaam
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya
mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa huduma ya mabasi
yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).
Akizungumza
leo na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es salaam akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema
Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi ambapo
nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi Kariakoo shilingi
1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi 1400 na wanafunzi watatozwa
nusu ya viwango hivyo vya nauli.
Waziri
Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi huku mradi huo
ukiwa umelenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya jiji,
“Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi na wananchi ambao
hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha,
ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi ,
Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya
viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi
huo.
Tarehe
25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya
TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi Dar es salaam
(UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu ili mradi huo wa
mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10, Januari 2016, imebainika kwamba
UDART hawakuandaa mpango wa biashara wala kuanisha gharama za uendeshaji.
Chanzo cha habari : Ofisi ya Waziri Mkuu
Asante kwa kuendelea
kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Comments