BREAKING NEWS: DAR ES SALAAM JENGO LA WIZARA YA MAMBO YA NDANI MAKAO MAKUU YA JESHI LA POLISI TANZANIA LANUSURIKA KUTEKETEA KWA MOTO
Na.Issack Gerald-Dar es Salaam
Jengo la Wizara ya mambo ya ndani makao makuu ya
jeshi la Polisi,limenusulika kuteketea kwa moto na kusababisha kazi za jeshi
hilo kusimama kwa muda,kutokana na wafanyakazi na viongozi wa jeshi hilo kutoka
nje ya jengo kufuatia ya tahadhari ya moto kutolewa.
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Mratibu Mwandamizi wa Polisi, Tanzania Advera
Bulimba,amesema
kuwa cheche za moto zilianza kuonekana Ghorofa ya nne,ambapo hata hivyo moto
huo umedhibitiwa na kikosi jeshi la uokozi na zimamoto.
Comments