UELEWA MDOGO WA WATU WAISHIO NA VIRUSI VYA UKIMWI,BADO CHANGAMOTO KUUDHIBITI UGONJWA WA UKIMWI
Na.Issack Gerald-Mwanza
Muuguzi wa Kituo kinacho toa huduma
kwa watu wanaoishi na maambukizi ya Virus Vya UKIMWI na Yatima Shalom Care
House Jijini Mwanza Bi Edna Evarist
amesema uelewa mdogo wa watu wanaoishi
Na VVU ni changamoto katika kudhibiti UKIMWI nchini.
Bi Evaristi ameyasema hayo
wakati akizungumza na Redio Kwizera Juu
ya kauli mbiu ya taifa chini ya wizara ya afya na usitawi wa jamii kufikia
sufuri tatu katika kudhibiti maambukizi
mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na VVU Na unyanyapaa.
Amesema kuwa watu wenye virusi vya
UKIMWI wengi wao wamekuwa wakiendeleza maambukizi hayo kwa kuoa na kuolewa au
kuanziasha mahusiano mapya bila kuwahusisha wenzi wao huku wakijua hali zao
kiafya na kusababisha maambukizi ya
UKIMWI nchini kuendelea.
Aidha mratibu wa kituo hicho Bw
Msafiri Wana amesema kuwa Idadi ya watoto yatima kutokana na vifo vianavyo
sababishwa na Ukimwi imepungua baada ya jamii kujua umuhimu wa matumizi sahihi
ya dawa za punguza makali ya VVU.
Comments