JESHI LA POLISI KATAVI LASHAURIWA KUZUIA UHARIFU BADALA YA MATUKIO
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi la polisi mkoani Katavi
limeshauriwa kujenga desturi ya kuzuia uharifu kabla haujatokea badala ya
kupambana na matukio
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa
wa Katavi, Dr. Ibrahim Msengi wakati wa maadhimisho ya siku ya Polisi nchini
iliyofanyika Juzi katika viwanja vya Polisi Wilayani Mpanda.
Dr. Msengi amesisitiza kuwa endapo
jeshi la polisi litawatumia askari wake kufanya tafiti na kushirikisha wananchi
katika ukusanyaji wa taarifa, uharifu utadhibitiwa kabla haujaleta madhara.
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la
polisi mkoa wa Katavi ACP Dhahiri Kidavashari amekiri kuwepo kwa mafanikio
pamoja na changamoto ambazo zitafanyiwa kazi ili kuimarisha usalama.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi
Mkoani Katavi Dhihiri Kidavashari aliwapongeza wananchi wanaoendelea kuonesha
ushirikiano wa kuwabaini waharifu wa vitendo mbalimbali
Comments