AFISA ELIMU WILAYANI NKASI AELEZA MIKAKATI YA KUINUA KIWANGO CHA UFAULU WILYANI HUMO
Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
HALMASHAURI ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeazimia
kuongeza kiwango cha ufaulu kwa mwaka wa 2016.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA
sambamba na mpanda, Afisa elimu taaluma wilaya ya Nkasi Bw. George Muhenda amesema, kutakuwa na kikao kitakachohusisha
wadau wote wa elimu ili kujadili mbinu za kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka
asilimia 67.79 kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 82 mwaka huu.
Aidha Bw. Muhenda ameongeza kuwa,walimu
pia wanatakiwa kujituma bila shuruti ili kuboresha elimu.
Kwa upande wao walimu wilayani humo ambao wameshiriki mafunzo ya namna
ya kuongeza ufaulu katik masomo ya hesabu,Kiswahili na kiingereza wamesema bado
kuna changamoto ya miundombinu mibovu ya elimu ikiwemo upungufu wa
madarasa,madawati lakini pia ukosefu wa walimu wenye weledi wa kutosha kumudu
masomo kusika.
Hata hivyo Serikali ya Wilaya ya
Nkasi kwa ujumla imeiomba serikali kusaidia miundombinu mbalumbali ya madarasa
na nyumba za walimu ili matokeo makubwa sasa yapatikane kwa haraka zaidi.
Wiki iliypita,zaidi ya walimu 120
walishiriki mafunzo hayo ya kuinu akiwango cha ufaulu katika shule za msingi
ambapo jumla ya Halmshauri 8 za Wilaya zilihusishwa zikitokea mikoa ya
Kigoma,Rukwa na Katavi.
Comments