ASHIKILIWA NA POLISI KATAVI KWA KUKAMATWA NA METO YA TEMBO KILOGRAM 50 YENYE THAMANI YA SHILINGI MIL.120.
Na.Issack Gerald-Katavi
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) mkazi wa kijiji cha mbede anashikiliwa na Jeshi la Polisi akiwa na meno 08 ya tembo vyenye
uzito wa kg 50 ikiwa na thamani ya Tshs 120,000,000/= ambapo ni sawa na
tembo 4 waliouawa kinume
cha sheria.
Mtuhumiwa bw.Nzuri Ndizu akiwa Polisi kwa Mahojiano baada ya kukamatwa na meno ya tembo(PICHA na.Issack Gerald) |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi akifafanua kuhusu kukamatwa kwa mtuhumiwa wa meno ya tembo |
Meno ya tembo yaliyokamatwa haktika hatua ya kusubiri kuuzwa |
Akithibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amesema kuwa mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo mnamo tarehe 08.01.2016
majira ya saa 3 na nusu usiku kwenye pori la akiba la Lwafe Wilayani Mlele Mkoani
Katavi.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa,Jeshi la
Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuwa
kuna watu wanajihusisha na biashara haramu ya meno ya tembo na kuanza
kufuatilia taarifa hizo na hatimaye kumkamata mtuhumiwa Nzuri Ndizu akiwa na vielelezo hivyo vilivyokuwa vimefichwa
porini kusubili wateja.
Hata hivyo jeshi la polisi linaendela na
uchunguzi zaidi
kubaini mitandao yote inayojihusisha na
biashara hivyo haramu ya meno ya tembo ambapo mtuhumiwa atafikishwa afikishwa
mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Comments