MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA MWANZA AFA MAJI AKIWA NA BABAYE,ASKARI WA UOKOAJI WAKOSA MWILI
Na.Albert
Kavano-Mwanza
MWANAFUNZI
wa Darasa la Kwanza katika shule ya
Msingi Mabatini B Jijijni Mwanza Amefariki dunia baada ya kusombwa na maji
yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha jana kwa zaidi ya saa 6, jijini humo.
Tukio
hilo mlimetokea juzi majira ya saa nane mchana na kumhusisha Mtoto Janeth James
Joseph (6), aliyetumbukia katika Mto mirongo baada ya kuteleza wakati akijaribu
kuvuka akiwa na baba yake.
Akizungumzia
tukio hilo Mzazi wa Maerehemu Janeth, Bw James Joseph amesema kuwa ilikuwa ni
siku ya pili baada ya Mwanae kuanza masomo ya Darasa la kwanza katika shule ya
Msingi Mabatini B na kukutwa na ajari
hiyo wakati akitoka shule kurudi nyumbani.
Zoezi
la kuutafuta mwili wa mtoto huyo kupitia vikosi vya usalama na uokaji jijini
mwanza bado linaendelea na mpaka sasa Mwili huo haujapatikana .
Comments