AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SHAMBULIO LA MME WAKE
Na.Issack Gerald-Mpanda
MTU
mmoja mkazi wa Kawajense katika Manispaa ya Mpanda, Bi. Judith Mgawe, juzi
amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la
shambulio la kudhuru mwili dhidi ya mmewe.
Akisoma
shtaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela, Koplo Mtei wa
jeshi la polisi Mpanda amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 8 mwaka,
kwa kumpiga mmewe Bw. Kasanga Mgamba kwa kutumia kipande cha ubao na
kumsababishia maumivu makali..
Hakimu
Mbembela ameruhusu dhamana kwa mshtakiwa, lakini mshtakiwa alikosa mdhamini na
kulazimika kudhaminiwa na Bibi yake, baada ya mahakama hiyo kulinda maslahi ya
mtoto mdogo aliye naye.
Mshtakiwa
amekana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 3 mwezi Februari
mwaka huu itakaposikilizwa tena.
Comments