MATUKIO YA WIKI KATAVI NA KWINGINEKO KUANZIA JANUARI 11 – 16,2016 NA P5 TANZANIA MEDIA
Posted By:Issack Gerald
| At:Tuesday, January 12, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Nzuri Ndizu (44) mkazi wa kijiji cha mbede
anashikiliwa na Jeshi la Polisi akiwa na
meno 08 ya tembo vyenye uzito wa kg
50 ikiwa na thamani ya Tshs 120,000,000/= ambapo ni sawa na
tembo 4 waliouawa kinume
cha sheria.
Akithibitisha
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo,Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amesema kuwa mtuhumiwa huyo ametenda kosa hilo mnamo tarehe
08.01.2016 majira ya saa 3 na nusu usiku kwenye pori la akiba la Lwafe Wilayani
Mlele Mkoani Katavi.
Kamanda
Kidavashari amesema kuwa,Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema
kuwa katika pori la akiba la Lwafe kuwa kuna watu wanajihusisha na biashara
haramu ya meno ya tembo na kuanza kufuatilia taarifa hizo na hatimaye kumkamata
mtuhumiwa Nzuri Ndizu akiwa na vielelezo
hivyo vilivyokuwa vimefichwa porini kusubili wateja.
Hata
hivyo jeshi la polisi linaendela na uchunguzi zaidi
kubaini
mitandao yote inayojihusisha na biashara hivyo haramu ya meno ya tembo ambapo
mtuhumiwa atafikishwa afikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Posted By:Issack Gerald
| At:Monday, January 11, 2016
Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi
Naibu
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.William Tate Ole Nasha,amemwagiza
Mrajishi wa vyama vya ushirika Tanzania,kuhakikisha anaunda timu ya ukaguzi
ndani ya Siku 14 ili kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku katika
chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda Kati kilichopo Wilayani
Mpanda.
Waziri Nasha ametoa agizo hilo katika kikao ambacho
kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji Wilayani Mpanda kikishirikisha
Viongoz I wa vyama vya ushirika Mpanda Kati,Kaimu mrajishi Mkoa,Mkuu wa Wilaya
ya Mpanda na viongozi wengine waandamizi amabo amekuja nao kutoka Wizarani.
Akizungumza mbele ya wanachama zaidi ya 100 wa chama cha
ushirika Cha Mpanda Kati,Waziri Nasha ameonesha kutoridhishwa na majibu ya
uongozi wa ushirika Wilaya ya Mpanda kutokana na majibu yao kutokuonesha wazi
taarifa za malipo ya pesa za wakulima.
Katika malalamiko ya wakulima ni pamoja na kutolipwa pesa
zao kwa awamu tofauti kutokana tumbaku yao iliyouzwa,kupunjwa kwa pembejeo za
kilimo,kulipwa kwa Shilingi badala ya Dola kama wanavyoza na masuala mbalimbali
kama amvyo baadhi wamebaoinisha.
Hata hivyo,kufuatia kauli ya serikali kwa mrajisi wa vyama
vya ushirika Tanzania kumtaka kuunda timu ya uchunguzi,wakulima hao wamekuwa na
maoni Tofauti kuzungumzia hatua hiyo.
Kwa nyakati tofauti wakulima wa chama hicho cha msingi
wamekuwa wakilalamika kunyanayaswa kutokana na uuzaji wa tumbaku yao na malipo
wanayopewa kuanzia miaka ya 2010,ambapo
kwa mjibu wa wakulima wametaka kufahamu Jumla ya shilingi milioni 600 zilipo
ili walipwe pesa zao.
Hata hivyo Afisa ushirika Wilayani Mpanda Luxford Mbunda
amesema kuwa hakuna pesa wanayodai wakulima wala wakulima hao hakuna deni
wanalodaiwa ambapo ndicho chanzo cha sokomoko la sintofahamu juu ya upatikanaji wa pesa hizo.
Viongozi wa Wilaya na Mkoa licha ya kuwa wanatafuta ufumbuzi
wa mgogoro huo hakuna mafanikio yaliyopatikana.
Chama cha Msingi cha Ushirika cha Mpanda Kati,ni miongoni
mwa vyama saba vya msingi vinavyounda chama kikuu cha Ushirika LATCU Mkoani
Katavi.
Awali Waziri alipokea taarifa ya Mkoa katika sekta ya
kilimo,mifugo na uvuvi kabla ya kwenda katika ukumbi wa idara ya maji kaufanya
kikao na wakulima wa tumbaku chama cha Mpanda kati.
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA
JESHI LA POLISI KATAVI LASHAURIWA KUZUIA UHARIFU BADALA YA MATUKIO
Posted By:Issack Gerald
| At:Tuesday, January 12, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Jeshi
la polisi mkoani Katavi limeshauriwa kujenga desturi ya kuzuia uharifu kabla
haujatokea badala ya kupambana na matukio
Agizo
hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Katavi, Dr. Ibrahim Msengi wakati wa
maadhimisho ya siku ya Polisi nchini iliyofanyika Juzi katika viwanja vya
Polisi Wilayani Mpanda.
Dr. Msengi amesisitiza kuwa endapo jeshi la polisi
litawatumia askari wake kufanya tafiti na kushirikisha wananchi katika
ukusanyaji wa taarifa, uharifu utadhibitiwa kabla haujaleta madhara.
Kwa
upande wake mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi ACP Dhahiri Kidavashari
amekiri kuwepo kwa mafanikio pamoja na changamoto ambazo zitafanyiwa kazi ili
kuimarisha usalama.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi
Mkoani Katavi Dhihiri Kidavashari aliwapongeza wananchi wanaoendelea kuonesha
ushirikiano wa kuwabaini waharifu wa vitendo mbalimbali
Posted By:Issack Gerald
| At:Tuesday, January 12, 2016
Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
HALMASHAURI ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeazimia
kuongeza kiwango cha ufaulu kwa mwaka
wa 2016.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na mpanda, Afisa elimu taaluma wilaya ya
Nkasi Bw. George Muhenda amesema, kutakuwa na kikao kitakachohusisha
wadau wote wa elimu ili kujadili mbinu za kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka
asilimia 67.79 kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 82 mwaka huu.
Aidha
Bw. Muhenda ameongeza kuwa,walimu pia wanatakiwa kujituma bila shuruti ili
kuboresha elimu.
Kwa
upande wao walimu wilayani humo ambao
wameshiriki mafunzo ya namna ya kuongeza ufaulu katik masomo ya
hesabu,Kiswahili na kiingereza wamesema bado kuna changamoto ya miundombinu
mibovu ya elimu ikiwemo upungufu wa madarasa,madawati lakini pia ukosefu wa
walimu wenye weledi wa kutosha kumudu masomo kusika.
Hata
hivyo Serikali ya Wilaya ya Nkasi kwa ujumla imeiomba serikali kusaidia
miundombinu mbalumbali ya madarasa na nyumba za walimu ili matokeo makubwa sasa
yapatikane kwa haraka zaidi.
Wiki
iliypita,zaidi ya walimu 120 walishiriki mafunzo hayo ya kuinu akiwango cha
ufaulu katika shule za msingi ambapo jumla ya Halmshauri 8 za Wilaya
zilihusishwa zikitokea mikoa ya Kigoma,Rukwa na Katavi.
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE AMPA POLE
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, January 13, 2016
Na.Issack Gerald
WAZIRI
MKUU,Kassim Majaliwa amemtembelea na kuampa pole mke wa Baba wa
Taifa, Mama Maria Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe Leticia
Nyerere.
Akizungumza na mama Maria
alipomtembelea nyumbani kwake jana(Jumanne, Januari 12,2016), Msasani jijini
Dar es salaam, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Mama Maria Nyerere pamoja na
familia na kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu katika kipindi hiki
kigumu baada ya kuondokewa na mpendwa wao.
“Kipindi hiki ni kigumu, hatuna budi
kumshukuru Mungu kwa kila jambo, pia tutajumuika nanyi katika kipindi hichi
chote, tuendelee kuwa watulivu na kumwomba Mungu” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Ndugu wa marehemu, John Shibuda
(aliyewahi kuwa mbunge wa CHADEMA) ameeleza kutokea kwa msiba huo. Ambapo
amesema “Desemba, 19 mwaka huu Leticia Nyerere alipelekwa nchini Marekani kwa
matibabu na alifariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo
Lanham, Maryland juzi saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Aidha, Shibuda amemshukuru
Mheshimiwa Rais John Magufuli kwa kwenda kuipa pole familia na Serikali kwa
namna ambavyo inatoa ushirikiano mzuri kwa familia.
Naye, Rose Nyerere amesema familia
inaendelea na maaandalizi, hivyo watatoa taarifa ya baada ya kuandaa utaratibu
wa siku ambayo mwili utaletwa nchini, kuagwa na hatimaye kuzikwa Butiama.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye
ambaye amelazwa siku kadhaa zilizopita katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo
katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Majaliwa, amesema
amefarijika baada ya kumuona Waziri Mkuu huyo mstaafu akiendelea vizuri na
kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa kumpatia matibabu na kumhudumia vizuri.
Pamoja na kumpa pole, Waziri Mkuu amemwombea apone haraka ili aweze
kuendelea na majukumu yake ya kila siku.
Naye, Waziri Mkuu mstaafu Fredrick
Sumaye amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kumtembelea hospitalini hapo, pia ameipongeza
Serikali kwa jitihada mbalimbali inazofanya ili kusaidia wananchi na hatimaye
kuiletea nchi maendeleo.
“Naipongeza Serikali kwa namna
ambavyo inaendelea kutekeleza majukumu yake katika masuala mbalimbali yenye
lengo la kusaidia wananchi” alisema Sumaye.
Waziri Mkuu Majaliwa, pia
amemtembelea na kumjulia hali Balozi Hassan kibelloh ambaye amelazwa na
anaendelea kupatiwa matibabau katika Taasisi ya Jakaya Kikwete iliyopo katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Asante kwa kuendelea kuchagua P5 TANZANIA
MEDIA
Chanzo cha Habari: Ofisi ya Waziri mkuu
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, January 13, 2016
Na.Issack Gerald-Mwanza.
Jamii nchini imetakiwa
kutowanyanyapaa waathirika wa dawa kulevya badala yake iwasaidie kuondokana na
matumizi ya dawa hizo ikiwemo kuwafikisha katika vituo vya utimamu wa akili
(Sobar House).
Rai hiyo imetolewa Bw Eddy Darkis
Meneja wa Kituo cha Utimamu wa akili cha Back To Life Sobar House Pasiansi Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza,
ambacho husaidia wahanga wa dawa za kulevya kuachana na matumizi ya dawa hizo.
Bw Darkis amesema kuwa badhi ya
wanajamii wamekuwa wakiwanyanyapaa wahanga wa dawa za kulevya, jambo ambalo
linakwamisha mapambano dhidi ya matumizi ya dawa hizo nchini ambapo wahanga zaidi ya 50 wamepatiwa tiba huku wengine 25 wakiendelea
vizuri.
Ripoti ya Mwenyekiti wa chama cha
waandishi wa wa habari za kupiga vita uharifu, biashara na matumizi ya dawa za
kulevya nchini OJADACT Bw Edwini Soko Miezi 6 ili yopita,idadi ya watumiaji wa
dawa za kulevya Jijini Mwanza imefikia zaidi ya watu elfu kumi.
Asante kwa kuendelea kuchagua P5 TANZANIA MEDIA
Chanzo:Mwandishi wetu Mwanza
MAFURIKO YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, January 13, 2016
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Shule
ya Msingi Nsemulwa iliyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,mpaka sasa
imesajili Jumla ya wanafunzi 513 wa darasa la kwanza na Chekechea na
hatimaye kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa,madawati na matundu ya
vyoo.
Hayo
yamebainishwa na Afisa elimu kata ya Nsemulwa Bw.Gerigori John Mshota wakati
akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio shuleni hapo.
Amesema
kati ya wanafunzi 513,wanafunzi wa darasa la kwanza waliopo ni 318 huku chekechea wakiwa 195 na kufikia jumla ya
wanafunzi 1945 waliopo kati shule hiyo kwa sasa
ambapo kwa uwiano wa walimu 19 waliopo,kila mwalimu anatakiwa kufundisha
wanafunzi 102.
Amesema
changamoto zilizopo ni upungufu wa vyumba vya madarasa 6,madawati 504 ambapo
madarasa yaliyopo kwa sasa ni 7,mawati 200 huku matundu ya vyoo yakiwa 7.
Asubuhi
ya leo,P5 TANZANIA MEDIA Na Mpanda
Radio zimefika shuleni hapo na kushuhudia mwalimu mmoja akifundisha walimu 318
sababu kubwa ikitajwa kuwa na uhaba wa walimu.
Mwalimu
Joyce Mwandega ambaye ndiye
amekabidhiwa wanafunzi hao wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Nsemulwa
amezungumza na Mpanda Radio fm kutokana na hali iliyopo kuhusu wingi wa
wanafunzi katika shule hiyo.
Hata
hivyo ameiomba serikali na wadau wa elimu kusaidia kutatua changamoto za shule
hiyo ambapo kuna uwezekano wa wanafunzi wakafikia idadi ya zaidi ya 2000
watakaokuwa katika shule hiyo tofauti na siku zote.
Posted By:Issack Gerald
| At:Wednesday, January 13, 2016
Na.Issack Gerald
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amekuatana na kufanya mazungumzo na mabalozi wawili kutoka nchi za Qatar na
Kuwait.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na
mabalozi hao leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaam, Waziri Mkuu
amewashukuru mabalozi hao kwa pongeza walizokuja kumpatia, pamoja na namna
ambavyo nchi zao zimekua zikisaidia Tanzania, ambapo ameahidi kuendeleza
ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na nchi zao.
Kwa upande wake, Balozi wa Qatar, Abdallah Jassim
al Maadad amesema Serikali yake itaendelea kuisaidia Tanzania katika
maeneo yote ambayo Qatar imepiga hatua kubwa na inaweza kutoa msaada kwa
Tanzania.
Amesema Quwait iko tayari kuwekeza
nchini katika sekta ya kilimo, kwa vile ardhi ya Tanzania ni yenye rutuba
na inafaa kwa shughuli za kilimo. Aidha, ametaja sekta nyingine ambazo
wangependa kuwekeza ni pamoja na sekta ya uvuvi na viwanda.
Naye, Balozi wa Kuwait, Jasem Al Najem
ambaye amekuja kujitambulisha kwa Waziri Mkuu, amesema nchi yake kupitia
‘Kuwait fund’ iko tayari kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Balozi Najem, pia ameshauri vituo
vya uwekezaji vya Tanzania na Kuwait kufanya kazi kwa ushirikiano zaidi ili
kurahisisha utekelezaji wa miradi mbalimbali.
Chanzo cha Habari:Ofisi ya Waziri
Mkuu
BABA NA MAMA WA KAMBO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA MANYANYASO NA KUMNYIMA CHAKULA MTOTO WAO
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday, January 13, 2016
Na.Issack Gerald-KATAVI
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Ramadhani Charles (40) Mkazi wa Kasimba anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani
Katavi kwa kosa la kumnyanyasa mtoto wake anayeitwa Adam Ramadhani (17) ambaye
ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kashaulili sambamba na kumnyima mambo
mengine ya msingi kama chakula.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na Mpanda Radio, Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa Jeshi la Jeshi la polisi
limeshughulikia tatizo hilo la unyanyasaji baada ya kupokea taarifa kutoka
kituo cha matangazo ya Mpanda Radio FM.
Kamanda
Kidavashari amesema kuwa baada ya taarifa hiyo jeshi la polisi lilimpokea mtoto
huyo kituoni na kuanza kulifatia suala hilo ambapo mtoto huyo alieleza kuwa
alikuwa anaishi na baba yake mzazi na mama yake mlezi au wa kambo aitwaye Joyce
Sino.
Kwa
mjibu wa maelezo ya mtoto aliyenyanyaswa kwa nyakati tofauti alisema kuwa
manyanyaso yalianza mara baada ya mama yake kufariki ambapo awali waliishi
vizuri kabla ya kifo cha mama yake
lakini ghafla hali ilibadilika na akawa hapatiwi mahitaji ya kimaisha yakiwemo
mavazi, chakula, matibabu na mahitaji ya shule kutoka kwa wazazi wake licha ya
wazazi wake kupewa misaada kanisani na mwisho alifukuzwa na wazazi wake tarehe
29.12.2015 kwamba asikanyage kwake tena.
Baada
ya tukio hilo tarehe 31.12.2015 majira ya asubuhi jeshi la polisi lilituma hati
ya wito kwa baba mzazi wa mtoto ambaye baada ya kuipokea alikuja kituoni na
wenzake wawili kujihami kwa kufungua taarifa ya upotevu wa tarehe 01.01.2016.
Kufuati
hali hiyo,Jeshi la Polisi limefungua jalada la uchunguzi ambapo upelelezi
ulikamilika na kumfikisha mtuhumiwa Ramadhani Charles mahakamani kwa kesi ya
kushindwa kutoa mahitaji na uangalizi.
Kesi
ya mtu huyu inatarajiwa kutajwa tarehe 01.02.2016. pia, jitihada zinafanyika za
kumkamata Joyce Sino ili afikishwe mahakamani kwa kosa hilo hilo.
Hata
hivyo Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari ametoa wito kwa
wazazi kuacha vitendo vya unyanyasaji kabla hatua za kisheria hazijawakabidhi.
Mkoa
wa Katavi,ni miongoni mwa mikoa ambayo ukatiri umekuwa ukitokea kwa nyakati
tofauti.
Asante kwa kuchagu P5
TANZANIA MEDIA,Endelea kuhabarika
0 comments:
Posted By:Issack Gerald
| At:Thursday, January 14, 2016
Na.Boniface Mpagape-MPANDA
MKAZI
wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda, Bw. Reuben Remi amefikishwa katika
mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja duka na kuiba
nguo zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne na elfu arobaini.
Akisoma
shtaka hilo mahakamani hapo, Koplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda, ameiambia
mahakama kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo desemba 28 mwaka jana, ambapo
alivunja duka la Bi. Rosana Mwamicheta katika mtaa wa majengo mjini Mpanda.
Mbele
ya hakimu David Mbembela, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kuiomba
mahakama iruhusu dhamana.
Akitoa
masharti ya dhamana, hakimu Mbembela amesema, mshtakiwa anatakiwa awe na
wadhamini wawili ambao watawasilisha vitambulisho mahakamani, na mmoja kati yao
akabidhi dhamana ya fedha taslimu shilingi laki saba na elfu ishirini na
mwingine ahadi ya kiasi hicho cha fedha.
Kesi
hiyo itatajwa tena January 27 mwezi huu
na itaanza kusikilizwa january 28, na
Mshtakiwa amerudishwa rumande hadi masharti ya dhamana yatakapokamilika.
Wakati
huo huo,mkazi wa Kigamboni kata ya shanwe
katika manispaa ya Mpanda Fredrick Josephat (18) amefikishwa katika mahakama ya
Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja nyumba na kuiba vitu vya
ndani vyenye thamani ya shilingi laki tano na elfu sitini na saba.
Imeelezwa
mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 03 mwezi huu nyakati
za usiku, nyumbani kwa Bw. Didas Boniface ambapo baadhi ya vitu vilikutwa kwa
mshtakiwa.
Hata
hivyo, mshtakiwa Fredrick Josephat amekana kutenda kosa hilo.
Hakimu
David Mbembela amesema mshtakiwa ana haki ya dhamana au anaweza kujidhamini
mwenyewe kwa kutoa fedha nusu ya thamani ya vitu vilivyoibwa, au mdhamini awe
mtumishi wa serikali na atoe kitambulisho na ahadi ya kulipa fedha shilingi
laki tano na elfu sitini na saba.
Mshtakiwa
ameshindwa kutekeleza masharti hayo, na amerudishwa rumande hadi
atakapokamilika masharti hayo na Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 20 mwezi
huu.
Posted By:Issack Gerald
| At:Thursday, January 14, 2016
Na.Issack Gerald
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa
amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura.
Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Rwanda.
Akizungumza na Balozi
Kayihura jana jumatano ofisini kwake, Magogoni jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa kumtembelea na ameahidi kuwa
Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi hizi mbili.
“Nia yetu ni kushirikiana kwa pamoja
kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa kutumia Bandari ya Dar es
salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga kwa kiwango cha kisasa ‘standard
gauge’ ili ziweze kubeba mizigo mingi na kwenda mwendo wa kasi” alisema
Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Balozi wa Rwanda, Kayihura amesema
Tanzania na Rwanda ni nchi marafiki na zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko
tayari kushirikiana na Tanzania kikanda na kimataifa.
“Tunatumia Bandari ya Dar es salaam
na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo mnaboresha Bandari ya Dar es Salaam,
kwani Rwanda inafaidika pia kwa vile mizigo yetu mingi karibu asilimia 75
husafirishwa kupitia bandari hii” alisema Balozi Kayihura.
Posted By:Issack Gerald
| At:Friday, January 15, 2016
Na.Issack Gerald-MPANDA
Balaza
la madiwani Manispaa ya Mpanda limetoa kauli ya pamoja kuunga mkono Juhudi za
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe
Magufuli.
Kauli
hiyo ya Madiwani,imetolewa jana katika mkutano wa balaza la pili la madiwani
ambao umefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Kupitia
hicho kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili taarifa za kamati
mablimbali,baadhi ya masuala yaliyobainishwa ni pamoja na kujadili namna ya
kutatua changamoto zinazoathiri wakazi wa Manispaa ya Mpanda.
Baadhi
ya changamoto hizi ni Upungufu na
ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa kama vile kata za Mpanda
Hotel,baadhi ya maeneo ya Ilembo.
Changamoto
nyingine zilizopo ni,Huduma duni za afya katika Hospitali na Zahanati,Mapambano
dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi,miundombinu mibovu ya barabara
zilizopo katika mipaka ya Manispaa.
Awali
Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Mheshimiwa Willium Philipo Mbogo akifungua kikao hicho cha pili cha balaza
hilo kwa mwaka 2016 amesema kuwa miradi
mbalimbali inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita iliyosalia ya
mwaka wa fedha 2015/2016.
Pamoja
na mambo mengine,amesema, miradi hiyo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa
mapato ya ndani,kutatua changamoto za elimu kwa shule za Manispaa zikiwemo upungufu wa madawati
pamoja na na kutekeleza mipango ya serikali.
Hata
hivyo wajumbe katika balaza hilo,wameiomba manispaa kutatua changamoto za
migogoro ya ardhi na kuainisha thamani ya magari mawili ya Manispaa aina ya
Scania yanayotarajiwa kuuzwa mwaka huu 2016.
Wakati
huo huo Suala la ukosefu wa Maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Mpanda
limeonekana kuwakasirisha baadhi ya madiwani na hivyo kuhoji wajibu wa viongozi
waliopewa kusimamia usambazaji wa maji safi na salama ambao ni idara ya maji
MUWASA.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ambaye kisheria katika balaza la
madiwani ndiye katibu,ametoa rai kwa madiwani kusambaza elimu kwa wananchi ili
kuendeleza kupambana na maambukizi ya Ukimwi ambayo huenda kama takwimu
zikitolewa kuna uwezekano wa kuzidi asilimia 5.9 ya maambukizi ya Ukimwi kwa
sasa.
Katika
hatu a nyingine Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inatarajia kuuza magari
mawili aina ya Scania huku magari mengine yatakayouzwa hayajaainishwa ni magari
mangapi na aina gani.
Kwa
upande wa baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda wamesema kuwa miundombinu ya
afya,barabara,afya maji na migogoro ya ardhi inatakiwa kutatuliwa haraka.
Posted By:Issack Gerald
| At:Friday, January 15, 2016
Na.Issack Gerald-Mlele
Waziri
wa kilimo,mifugo na uvuvi Mheshimiwa Willium Tate Nashe,amewataka watumishi wa
umma Wilayani Mlele Mkoani Katavi kufanya kazi kwa uadilifu,uaminifu sambamba
na kuwa karibu na wananchi kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili
wananchi hao.
Waziri
Nashe ametoa wito huo jana, alipokuwa akizungumza na watumishi wa sekta
mbalimbali Wilayani Mlele katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
Aidha,Nashe
baada ya kikao na watumishi wa Umma,aliendelea kuzungumza na Chama cha msingoi
cha Ushirika cha Ukonongo kinachojishughulisha na kilimo cha tumbaku.
Amebainisha
malengo makuu ya ziara yake aliyoianza Jumatatu ya Januari 11 mwaka huu,Mkoani
Katavi kuwa ni kwa ajili ya kuja kutatua changamoto za wakulima zinazowakabili
katika sekta ya kilimo,ardhi,ufugaji na uvuvi.
Wakati
huo huo,ameupongeza mkoa wa Katavi kwa kuwa miongoni mwa mikoa ambayo haina
historia ya njaa kwa kuwa Mkoa wa Katavi unalisha maeneo mengine yaliyokumbwa
na njaa ikiwemo Shinyanga.
Waziri
anaendelea na ziara ambapo leo ni siku ya tano tangu aanze ziara Mkoani Katavi
ambapo ameelekea Wilayani Mlele akitokea Wilayani Mpanda baada ya kupata
taarifa ya Mkoa ya maendeleo ya kilimo,mifungo na uvuvi na hatimaye kuzungumza
na wakulima wa tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda kati.
Posted By:Issack Gerald
| At:Friday, January 15, 2016
Na.Issack Gerald-Mpanda
Halmashauri
ya Manispaa ya Mpanda imesema kuwa mchakato wa kuhamisha Hospitali ya Wilaya ya
Mpanda kutoka katika utawala wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kuwekwa katika
utawala wa Manispaa unaendelea.
Hayo
yamebainishwa na mganga mkuu wa Manispaa Dk.Obed Mahenge kupitia kikao cha
balaza la madiwani ambacho kimefanyika jana katika ukumbi wa Manispaa ya
Mpanda.
Kutokana
na Manispaa kutokuwa na Hospitali yake ya Manispaa,Wajumbe wa kikoa wameiomba
manispaa ya Mpanda mchakato wa kuhamisha hospitali katika utawal mmoja kwenda
utawala mwingine ufanyike kwa haraka ili kuwaondolea adha wananchi.
Kwa
upande wake afisa anayehusika na ukusanyaji wa damu salama Manispaa ya Mpanda
Bi.Redgunda Mayorwa,amesem akuwa kipindi cha
mwezi Desemba mwaka jana hadi Mwezi Januari mwaka huu,amesem akuwa kiasi
ch adamu kilichokusanywa ni UNIT 407.
Katika
hatua nyingine ,Dk.Mahenge amesema kuwa kata ya Kakese imeendelea kupata
ongezeko la watu wenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ambapo kwa kipindi cha
mwezi Desemba mwaka 2015 hadi Januari mwaka huu,zaidi ya watu 40 wamegundulika
kuathirika.
Hata
hivyo wadau mbalimbali wameshauri kuwa,kondomu,elimu ya kutosha kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali viendelee kutolewa kwa wakazi wote wa Mkoa wa
Katavi.
Mkoa
wa Katavi una asilimia 5.9 ya maambukizi ambapo imevuka kiwango cha asilimia
kwa taifa,ambapo maambukizi asilimia ya maambukizi ni salimia 5.1.
Hata
hivyo kuna uwezekano wa aslimia kuongezeka ikiwa utafiti wa vipimo vya uhakika
utafanyika kwa kumekuwa na ongezeko la watu wengi kutoka maeneo mbalimbali ya
Tanzania Kuingia Mkoani Katavi.
AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA SHAMBULIO LA MME WAKE
Na.Issack Gerald-Mpanda
MTU
mmoja mkazi wa Kawajense katika Manispaa ya Mpanda, Bi. Judith Mgawe, juzi
amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la
shambulio la kudhuru mwili dhidi ya mmewe.
Akisoma
shtaka hilo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Bw. David Mbembela, Koplo Mtei wa
jeshi la polisi Mpanda amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo January 8 mwaka,
kwa kumpiga mmewe Bw. Kasanga Mgamba kwa kutumia kipande cha ubao na
kumsababishia maumivu makali..
Hakimu
Mbembela ameruhusu dhamana kwa mshtakiwa, lakini mshtakiwa alikosa mdhamini na
kulazimika kudhaminiwa na Bibi yake, baada ya mahakama hiyo kulinda maslahi ya
mtoto mdogo aliye naye.
Mshtakiwa
amekana shtaka hilo na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 3 mwezi Februari
mwaka huu itakaposikilizwa tena.
MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA MWANZA AFA MAJI AKIWA NA BABAYE,ASKARI WA
UOKOAJI WAKOSA MWILI
Na.Albert Kavano-Mwanza
MWANAFUNZI
wa Darasa la Kwanza katika shule ya
Msingi Mabatini B Jijijni Mwanza Amefariki dunia baada ya kusombwa na maji
yaliyotokana na mvua kubwa iliyonyesha jana kwa zaidi ya saa 6, jijini humo
Tukio
hilo mlimetokea juzi majira ya saa nane mchana na kumhusisha Mtoto Janeth James
Joseph (6), aliyetumbukia katika Mto mirongo baada ya kuteleza wakati akijaribu
kuvuka akiwa na baba yake.
Akizungumzia
tukio hilo Mzazi wa Maerehemu Janeth, Bw James Joseph amesema kuwa ilikuwa ni
siku ya pili baada ya Mwanae kuanza masomo ya Darasa la kwanza katika shule ya
Msingi Mabatini B na kukutwa na ajari
hiyo wakati akitoka shule kurudi nyumbani.
Zoezi
la kuutafuta mwili wa mtoto huyo kupitia vikosi vya usalama na uokaji jijini
mwanza bado linaendelea na mpaka sasa Mwili huo haujapatikana .
Asante kwa kuchagua P5
TNZANIA MEDIA
Kwa manoni tuma kwenda
geraldissack@gmail.com
Comments