WAWILI MANISPAA YA MAPANDA WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA WAKITHUMIWA KUIBA NAKUPORA MALI ZENYET THAMANI KARIBU MIL.2.


Na.Boniface Mpagape-MPANDA
MKAZI wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda, Bw. Reuben Remi amefikishwa katika mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja duka na kuiba nguo zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne na elfu arobaini.

Akisoma shtaka hilo mahakamani hapo, Koplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda, ameiambia mahakama kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo desemba 28 mwaka jana, ambapo alivunja duka la Bi. Rosana Mwamicheta katika mtaa wa majengo mjini Mpanda.
Mbele ya hakimu David Mbembela, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kuiomba mahakama iruhusu dhamana.
Akitoa masharti ya dhamana, hakimu Mbembela amesema, mshtakiwa anatakiwa awe na wadhamini wawili ambao watawasilisha vitambulisho mahakamani, na mmoja kati yao akabidhi dhamana ya fedha taslimu shilingi laki saba na elfu ishirini na mwingine ahadi ya kiasi hicho cha fedha.
Kesi hiyo itatajwa tena January  27 mwezi huu na itaanza kusikilizwa january 28, na  Mshtakiwa amerudishwa rumande hadi masharti ya dhamana yatakapokamilika.        
Wakati huo huo,mkazi wa Kigamboni kata ya shanwe katika manispaa ya Mpanda Fredrick Josephat (18) amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja nyumba na kuiba vitu vya ndani vyenye thamani ya shilingi laki tano na elfu sitini na saba.
Imeelezwa mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 03 mwezi huu nyakati za usiku, nyumbani kwa Bw. Didas Boniface ambapo baadhi ya vitu vilikutwa kwa mshtakiwa.
Hata hivyo, mshtakiwa Fredrick Josephat amekana kutenda kosa hilo.
Hakimu David Mbembela amesema mshtakiwa ana haki ya dhamana au anaweza kujidhamini mwenyewe kwa kutoa fedha nusu ya thamani ya vitu vilivyoibwa, au mdhamini awe mtumishi wa serikali na atoe kitambulisho na ahadi ya kulipa fedha shilingi laki tano na elfu sitini na saba.
Mshtakiwa ameshindwa kutekeleza masharti hayo, na amerudishwa rumande hadi atakapokamilika masharti hayo na Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 20 mwezi huu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA