MABALAZA YA MADIWANI MPANDA KUANZA VIKAO VYAKE LEO


Na.Issack Gerald-Mpanda
Balaza la madiwani Manispaa ya Mpanda leo linatarajia kuanza vikao vyake kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya wananchi.
                                            
Moja ya mambo yanayoifanya Mpanda kupewa Manispaa ya Mpanda

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA,mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mheshimiwa Willium Philipo Mbogo,amesema kuwa pamoja na kujadili masuala mbalimbali,pia wanatarajia kuchagua kamati mbalimbali zitakazokuwa chini ya balaza la madiwani kwa ajili ya kusimamia shughuliza maendeleo.
Manispaa ya Mpanda,ni manispaa ambayo inakabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo miundombinu mibovu ya barabara zinazotoka mjini kuelekea vijijini,Upungufu wa miundombinu ya elimu shuleni kama madarasa,upungufu wa walimu,huduma duni za afya katika hospitali ya Wilaya,Zahanati na vituo mbalimbali vya afya,ukosefu wa maji safi na salama katika maeneo mbali,mbali ya mji ikiwemo mtaa wa Mpanda Hotel  Kata ya Mpanda Hotel ulipo katikati ya Manispaa.
Wakati Manispaa ikifanya kikao chake,Wakati huo huo pia balaza la madiwani kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda watakuwa na kikao kama hicho,
Aidha changamoto zilizopo katika Halmashauri hiyo ni Miundombinu mibovu ya barabara hali inayopelekea wakulima kushindwa kutoa mazao shambani kupeleka mjini,ukosefu wa huduma za afya kwa baadhi ya maeneo.
Hata hivyo Halmashauri hii ni miongoni mwa Halmashauri ambazo zimekuwa zikivuka lengo la makusanyao ya mapato ya ndani hadi asiliamia 100 huku wakazi wa halmashauri hiyo wakiendelea  kupinga kelele kwa changamoto zinazowadhibiti.
Mshirikishe mwenzako asikose habari kemkem za Katavi na Kwingineko kupitia P5 TANZANIA MEDIA.Endelea kufuatilia kitakachojili katika mabalaza ya madiwani Katavi

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA