KIJIJI CHA MAJALILA SASA MAKAO MAKUU RASMI YA HALMASHAURI YA WILAYA MPYA YA TANGANYIKA



Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika
Kijiji cha Majalila kilichopo kata ya Tongwe Halmshauri Mpya ya Tanganyika Mkoani Katavi, kimetangazwa Rasmi kuwa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika.

Taarifa ya kijiji hicho kutangazwa kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika imetolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Amesema kuwa ametangaza ili kumaliza mvutano uliokuwepo kwa muda mrefu kwa serikali ya Halmshauri ya Tangaznyika(Zamani ikiitwa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda) ili kuondoa mvutano uliokuwepo hususani miongoni mwa madiwani ambao ni miongoni mwa viongozi wenye nguvu katika Halmshauri kupanga masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo.
Jenerali Muhuga amesema vijiji hatua ya kutangazwa kijiji cha Majalila ni baada kikao cha kamati ya ushauri  ngazi ya Wilaya iliyojadiliwa na madiwani ambapo vijiji vilivyokuwa katika mchakato wa kuchaguliwa kuwa makao Makuu ya Halmshauri ya Wilaya ni Majalila,Kamikusu na Migengebe.
Amesema kila kijiji kilitakiwa kiwe na vigezo 11 ambavyo ni  pamoja na uarahisi wa eneo hilo kufikika,upatikana ji wa huduma za kijamii,uwepo wa miundombinu za uhakika kama vile maji,barabara na mawasiliano,kuzingatia uhifadhi wa mazingira,ulinzi na usalama wa eneo hilo na mtawanyiko wa wakazi katika eneo hilo.
Wilaya ya Tanganyika ilitangazwa rasmi na serikali Feberuari 4,2016  kwa tangazo la serikali namba 68 ambapo wilaya hii inaundwa na tarafa 3,kata 16 pamoja na vijiji 55 ambapo mchakato ulipamba moto rasmi mwaka 2014 lakini kabla ya mchakato wa awali kuanzawaka 2004.
Kijiji cha Majalila kimeonekana kuwa na sifa nyingi kuliko vijjiji vya  Kamikusu na Migengebe.
 SIFA YA KIJIJI CHA MGENGEBE
-Kipo km 78 kutoka Mpanda Mjini
-Eneo hili lipo karibu na ushoroba wa hifadhi za wanayama kutoka hifadhi ya Katavi kwenda hifadhi ya mahale Kigoma.
-Si rahisi kufikika
-Lipo katika chanzo cha maji Katuma hivyo uharibifu wa vyanzo vya maji utafanyika
-Kijiji kina leseni 8 za uchimbaji wa madini
-Gharama za ujenzi zitakuwa kubwa kutokana na jiografia ya mahali kijiji kilipo.
SIFA YA KIJIJI CHA KAMIKUSU
-Kijiji hiki kipo km 20 kutoka barabara ya Mpanda-Uvinza
-Ni eneo ambalo kipindio cha masika huwa tepetepe ambapo hakuna majengo makubwa yanayowezekana kujengwa.
-Kipo katikati ya mito miwili ambapo vyanzo hivyo vya maji vitaharibika.
-Kuna wakazi wachache ambao watahitaji kulipwa fidia ya shilingi milioni 500 ili kupisha ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri.
SIFA YA KIJIJI CHA MAJALILA
-Kuna eneo la Heka 50 ambazo zimetolewa na wananchi bila fidia
-Eneo hilo linafikika kwa urahisi kutokana na kuwa kandokando ya barabara kuu kutoka Mpanda Kigoma.
-Kuna miradi wa maji wa matenki mawili ambao umezinduliwa na mwenge wa uhuru.
-Wapo wananchi zaidi ya 3000 watakaonufaika na mradi wa maji
-Kijiji cha Majalila ni eneo ambalo lipo katika Mpango wa kunufaika na umeme wa REA(Wakala wa umeme vijijini)
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo Mashama
Endelea kuhabarika na ‘’P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM’’

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA