WALIMU MKOANI KATAVI WATAKIWA KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA UTAPELI UNAOWAANDAMA,WALIMU WASTAAFU WAPEWA MSAADA WA MABATI 120



Na.Judica Schone-Mpanda
WALIMU mkoani Katavi wametakiwa kuepuka kutapeliwa na watu  wanaowalaghai pindi wanapopata mafao yao.

Rai hiyo imetolewa na afisa elimu mkoa wa katavi Bw.Ernest Hinju katika hafla ya kukabidhi zawadi ya mabati 120   yenye thamani ya sh.million 2 na laki 4 kwa walimu wastaafu 6  kutoka halmashauri ya Mpanda na manispaa ya Mpanda .
Aidha  Bw. Hinju amewataka wastaafu hao kuendeleza maisha waliyokuwa wakiishi wakiwa kazini na kutoiga maisha ya kigeni ambayo baadae yataleta madhara kwao.
Kwa upande wao walimu wastaafu wameshukuru ungozi wa chama cha walimu mkoa wa katavi kwa moyo wa uzalendo walionao na kuahidi kuyatekeleza yote waliyowahusia na kutodhalilisha kazi yao kwani ni muhimu sana.
Hata hivyo katibu wa chama cha walimu mkoa wa katavi Bi Lucy Masegenya amesema chama hicho kijimejipanga kutoa somo la ujasiliamali kwa walimu mara baada ya masaa ya kazi kuisha ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA