BALAZA LA MADIWANI MPANDA LAUNGA MKONO JUHUDI ZA RAIS MAGUFULI,WAPOKEA TAARIFA NA KUJADILI CHANGAMOTO ZA WANANCHI.


Na.Issack Gerald-MPANDA
Balaza la madiwani Manispaa ya Mpanda limetoa kauli ya pamoja kuunga mkono Juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dk.John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo ya Madiwani,imetolewa jana katika mkutano wa balaza la pili la madiwani ambao umefanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda.
Kupitia hicho kilichokuwa kinalenga kupokea na kujadili taarifa za kamati mablimbali,baadhi ya masuala yaliyobainishwa ni pamoja na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazoathiri wakazi wa Manispaa ya Mpanda.
Baadhi ya  changamoto hizi ni Upungufu na ukosefu wa maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa kama vile kata za Mpanda Hotel,baadhi ya maeneo ya Ilembo.
Changamoto nyingine zilizopo ni,Huduma duni za afya katika Hospitali na Zahanati,Mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi,miundombinu mibovu ya barabara zilizopo katika mipaka ya Manispaa.
Awali Mstahiki meya wa Manispaa ya Mpanda Mheshimiwa Willium Philipo Mbogo  akifungua kikao hicho cha pili cha balaza hilo kwa mwaka 2016  amesema kuwa miradi mbalimbali inatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita iliyosalia ya mwaka  wa fedha 2015/2016.
Pamoja na mambo mengine,amesema, miradi hiyo ni pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani,kutatua changamoto za elimu kwa shule  za Manispaa zikiwemo upungufu wa madawati pamoja na na kutekeleza mipango ya serikali.
Hata hivyo wajumbe katika balaza hilo,wameiomba manispaa kutatua changamoto za migogoro ya ardhi na kuainisha thamani ya magari mawili ya Manispaa aina ya Scania yanayotarajiwa kuuzwa mwaka huu 2016.
Wakati huo huo Suala la ukosefu wa Maji kwa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Mpanda limeonekana kuwakasirisha baadhi ya madiwani na hivyo kuhoji wajibu wa viongozi waliopewa kusimamia usambazaji wa maji safi na salama ambao ni idara ya maji MUWASA.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ambaye kisheria katika balaza la madiwani ndiye katibu,ametoa rai kwa madiwani kusambaza elimu kwa wananchi ili kuendeleza kupambana na maambukizi ya Ukimwi ambayo huenda kama takwimu zikitolewa kuna uwezekano wa kuzidi asilimia 5.9 ya maambukizi ya Ukimwi kwa sasa.
Katika hatu a nyingine Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda inatarajia kuuza magari mawili aina ya Scania huku magari mengine yatakayouzwa hayajaainishwa ni magari mangapi na aina gani.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi Manispaa ya Mpanda wamesema kuwa miundombinu ya afya,barabara,afya maji na migogoro ya ardhi inatakiwa kutatuliwa haraka.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA