WAZIRI WA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI ZIARANI MLELE,ATOA RAI KWA WATUMISHI WA UMMA,AZUNGUMZA NA WAKULIMA WA TUMBAKU


Na.Issack Gerald-Mlele
Waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi Mheshimiwa Willium Tate Nashe,amewataka watumishi wa umma Wilayani Mlele Mkoani Katavi kufanya kazi kwa uadilifu,uaminifu sambamba na kuwa karibu na wananchi kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili wananchi hao.

Waziri Nashe ametoa wito huo jana, alipokuwa akizungumza na watumishi wa sekta mbalimbali Wilayani Mlele katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele.
Aidha,Nashe baada ya kikao na watumishi wa Umma,aliendelea kuzungumza na Chama cha msingoi cha Ushirika cha Ukonongo kinachojishughulisha na kilimo cha tumbaku.
Amebainisha malengo makuu ya ziara yake aliyoianza Jumatatu ya Januari 11 mwaka huu,Mkoani Katavi kuwa ni kwa ajili ya kuja kutatua changamoto za wakulima zinazowakabili katika sekta ya kilimo,ardhi,ufugaji na uvuvi.
Wakati huo huo,ameupongeza mkoa wa Katavi kwa kuwa miongoni mwa mikoa ambayo haina historia ya njaa kwa kuwa Mkoa wa Katavi unalisha maeneo mengine yaliyokumbwa na njaa ikiwemo Shinyanga.
Waziri anaendelea na ziara ambapo leo ni siku ya tano tangu aanze ziara Mkoani Katavi ambapo ameelekea Wilayani Mlele akitokea Wilayani Mpanda baada ya kupata taarifa ya Mkoa ya  maendeleo ya  kilimo,mifungo na uvuvi na hatimaye kuzungumza na wakulima wa tumbaku wa chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda kati.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA