MRAJISI VYAMA VYA MSINGI TANZANIA APEWA SIKU 14 KUUNDA TIMU YA UKAGUZI MALALAMIKO YA WAKULIMA WA TUMBAKU MPANDA


Na.Issack Gerald-Mpanda,Katavi
Naibu Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Mh.William Tate Ole Nasha,amemwagiza Mrajishi wa vyama vya ushirika Tanzania,kuhakikisha anaunda timu ya ukaguzi ndani ya Siku 14 ili kuchunguza malalamiko ya wakulima wa zao la tumbaku katika chama cha msingi cha ushirika cha Mpanda Kati kilichopo Wilayani Mpanda.  
                                               
Wa-tatu kutoka kushoto aliyeshika kifuani mwake ni Naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa Wilaya ya Mpanda Muda mfupi kabla ya kuanza kikao na wakulima Chama cha Msingi Mpanda Katati,aliyevaa kaunda suti ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima na wengine katika picha ni wakuu wa idara Wilayani Mpanda
                                            


Waziri Nasha ametoa agizo hilo katika kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji Wilayani Mpanda kikishirikisha Viongoz I wa vyama vya ushirika Mpanda Kati,Kaimu mrajishi Mkoa,Mkuu wa Wilaya ya Mpanda na viongozi wengine waandamizi amabo amekuja nao kutoka Wizarani.
Akizungumza mbele ya wanachama zaidi ya 100 wa chama cha ushirika Cha Mpanda Kati,Waziri Nasha ameonesha kutoridhishwa na majibu ya uongozi wa ushirika Wilaya ya Mpanda kutokana na majibu yao kutokuonesha wazi taarifa za malipo ya pesa za wakulima.
Katika malalamiko ya wakulima ni pamoja na kutolipwa pesa zao kwa awamu tofauti kutokana tumbaku yao iliyouzwa,kupunjwa kwa pembejeo za kilimo,kulipwa kwa Shilingi badala ya Dola kama wanavyoza na masuala mbalimbali kama amvyo baadhi wamebaoinisha.
Hata hivyo,kufuatia kauli ya serikali kwa mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania kumtaka kuunda timu ya uchunguzi,wakulima hao wamekuwa na maoni Tofauti kuzungumzia hatua hiyo.
Kwa nyakati tofauti wakulima wa chama hicho cha msingi wamekuwa wakilalamika kunyanayaswa kutokana na uuzaji wa tumbaku yao na malipo wanayopewa kuanzia miaka  ya 2010,ambapo kwa mjibu wa wakulima wametaka kufahamu Jumla ya shilingi milioni 600 zilipo ili walipwe pesa zao.
Hata hivyo Afisa ushirika Wilayani Mpanda Luxford Mbunda amesema kuwa hakuna pesa wanayodai wakulima wala wakulima hao hakuna deni wanalodaiwa ambapo ndicho chanzo cha sokomoko la  sintofahamu juu ya upatikanaji wa pesa hizo.
Viongozi wa Wilaya na Mkoa licha ya kuwa wanatafuta ufumbuzi wa mgogoro huo hakuna mafanikio yaliyopatikana.
Chama cha Msingi cha Ushirika cha Mpanda Kati,ni miongoni mwa vyama saba vya msingi vinavyounda chama kikuu cha Ushirika LATCU Mkoani Katavi.
Awali Waziri alipokea taarifa ya Mkoa katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi kabla ya kwenda katika ukumbi wa idara ya maji kaufanya kikao na wakulima wa tumbaku chama cha Mpanda kati.
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA MEDIA

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA