BABA NA MAMA WA KAMBO WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MAKOSA YA MANYANYASO NA KUMNYIMA CHAKULA MTOTO WAO


Na.Issack Gerald-KATAVI
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ramadhani Charles (40) Mkazi wa Kasimba anashikiliwa na jeshi la Polisi Mkoani Katavi kwa kosa la kumnyanyasa mtoto wake anayeitwa Adam Ramadhani (17) ambaye ni mwanafunzi wa shule ya Sekondari Kashaulili sambamba na kumnyima mambo mengine ya msingi kama chakula.

 Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Sambamba na  Mpanda Radio, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amesema kuwa Jeshi la Jeshi la polisi limeshughulikia tatizo hilo la unyanyasaji baada ya kupokea taarifa kutoka kituo cha matangazo ya Mpanda Radio FM.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa baada ya taarifa hiyo jeshi la polisi lilimpokea mtoto huyo kituoni na kuanza kulifatia suala hilo ambapo mtoto huyo alieleza kuwa alikuwa anaishi na baba yake mzazi na mama yake mlezi au wa kambo aitwaye Joyce Sino.
Kwa mjibu wa maelezo ya mtoto aliyenyanyaswa kwa nyakati tofauti alisema kuwa manyanyaso yalianza mara baada ya mama yake kufariki ambapo awali waliishi vizuri  kabla ya kifo cha mama yake lakini ghafla hali ilibadilika na akawa hapatiwi mahitaji ya kimaisha yakiwemo mavazi, chakula, matibabu na mahitaji ya shule kutoka kwa wazazi wake licha ya wazazi wake kupewa misaada kanisani na mwisho alifukuzwa na wazazi wake tarehe 29.12.2015 kwamba asikanyage kwake tena.
Baada ya tukio hilo tarehe 31.12.2015 majira ya asubuhi jeshi la polisi lilituma hati ya wito kwa baba mzazi wa mtoto ambaye baada ya kuipokea alikuja kituoni na wenzake wawili kujihami kwa kufungua taarifa ya upotevu wa tarehe 01.01.2016.
Kufuati hali hiyo,Jeshi la Polisi limefungua jalada la uchunguzi ambapo upelelezi ulikamilika na kumfikisha mtuhumiwa Ramadhani Charles mahakamani kwa kesi ya kushindwa kutoa mahitaji na uangalizi.
Kesi ya mtu huyu inatarajiwa kutajwa tarehe 01.02.2016. pia, jitihada zinafanyika za kumkamata Joyce Sino ili afikishwe mahakamani kwa kosa hilo hilo. 
Hata hivyo Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari ametoa wito kwa wazazi kuacha vitendo vya unyanyasaji kabla hatua za kisheria hazijawakabidhi.
Mkoa wa Katavi,ni miongoni mwa mikoa ambayo ukatiri umekuwa ukitokea kwa nyakati tofauti.
Asante kwa kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Endelea kuhabarika

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA