MAFURIKO YA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA


Na.Issack Gerald-MPANDA
Shule ya Msingi Nsemulwa iliyopo kata ya Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,mpaka sasa imesajili  Jumla ya wanafunzi  513 wa darasa la kwanza na Chekechea na hatimaye kukabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa,madawati na matundu ya vyoo.

Hayo yamebainishwa na Afisa elimu kata ya Nsemulwa Bw.Gerigori John Mshota wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio shuleni hapo.
Amesema kati ya wanafunzi 513,wanafunzi wa darasa la kwanza waliopo ni 318 huku  chekechea wakiwa 195 na kufikia jumla ya wanafunzi 1945 waliopo kati shule hiyo kwa sasa  ambapo kwa uwiano wa walimu 19 waliopo,kila mwalimu anatakiwa kufundisha wanafunzi  102.
Amesema changamoto zilizopo ni upungufu wa vyumba vya madarasa 6,madawati 504 ambapo madarasa yaliyopo kwa sasa ni 7,mawati 200 huku matundu ya vyoo yakiwa 7.
Asubuhi ya leo,P5 TANZANIA MEDIA Na Mpanda Radio zimefika shuleni hapo na kushuhudia mwalimu mmoja akifundisha walimu 318 sababu kubwa ikitajwa kuwa na uhaba wa walimu.
Mwalimu Joyce Mwandega ambaye ndiye amekabidhiwa wanafunzi hao wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Nsemulwa amezungumza na Mpanda Radio fm kutokana na hali iliyopo kuhusu wingi wa wanafunzi katika shule hiyo.
Hata hivyo ameiomba serikali na wadau wa elimu kusaidia kutatua changamoto za shule hiyo ambapo kuna uwezekano wa wanafunzi wakafikia idadi ya zaidi ya 2000 watakaokuwa katika shule hiyo tofauti na siku zote.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA