AFISA ELIMU WILAYANI NKASI AELEZA MIKAKATI YA KUINUA KIWANGO CHA UFAULU WILYANI HUMO


Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
HALMASHAURI  ya wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa imeazimia kuongeza kiwango cha ufaulu   kwa mwaka wa 2016.

Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na mpanda, Afisa elimu taaluma wilaya ya Nkasi  Bw. George Muhenda  amesema, kutakuwa na kikao kitakachohusisha wadau wote wa elimu ili kujadili mbinu za kuongeza kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 67.79 kwa mwaka 2015 na kufikia asilimia 82 mwaka huu.
Aidha Bw. Muhenda ameongeza kuwa,walimu pia wanatakiwa kujituma bila shuruti ili kuboresha elimu.
Kwa upande wao walimu  wilayani humo ambao wameshiriki mafunzo ya namna ya kuongeza ufaulu katik masomo ya hesabu,Kiswahili na kiingereza wamesema bado kuna changamoto ya miundombinu mibovu ya elimu ikiwemo upungufu wa madarasa,madawati lakini pia ukosefu wa walimu wenye weledi wa kutosha kumudu masomo kusika.
Hata hivyo Serikali ya Wilaya ya Nkasi kwa ujumla imeiomba serikali kusaidia miundombinu mbalumbali ya madarasa na nyumba za walimu ili matokeo makubwa sasa yapatikane kwa haraka zaidi.
Wiki iliypita,zaidi ya walimu 120 walishiriki mafunzo hayo ya kuinu akiwango cha ufaulu katika shule za msingi ambapo jumla ya Halmshauri 8 za Wilaya zilihusishwa zikitokea mikoa ya Kigoma,Rukwa na Katavi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA