UDSM YAENDESHA KONGAMANO LA TAFAKURI YA UCHAUZI WA MWAKA 2015,MENGI YAIBULIWA.
Na.Mwandishi wetu-Dar es salaam
Watanzania wametakiwa kuacha ushabiki
wa vyama vya siasa na badala yake wajikite kutatua matatizo ya kitaifa.
Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jajji Joseph Sinde Warioba |
Hayo yamebainishwa leo na Waziri Mkuu
Mstaafu Jaji Josefu Sinde Warioba katika kongamamno la tafakuri ambalo limefanyika
Katika ukumbi wa chuo kikuu cha Dar es salaa wakijadili hoja mbalimbali ikiwemo
uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2015.
Jaji Warioba amesema kuwa ni lazima
kuondoa matatizo ya Rushwa,ukabila,udini huku akiwataka watanzania kuchagua
viongozi wanaoona matatizo ya kitaifa kuliko kuchagua viongozi wanaojali
masuala ya vyama vyao.
Hata hivyo baadhi ya wajumbe wa
kongamano hilo,waligusia mambo mbalimbali yakiwemo yanayohusu siasa kipindi cha
uchaguzi mwaka 2015,nafasi ya vyombo vya habari katika uchaguzi wa mawaka 2015
katika kuripoti hali ya uchaguzi,majukumu ya viongozi wa kitaifa kama
rais,mawaziri ,tume ya taifa ya Uchaguzi na katiba ya Tanzania.
Kuhusu Katiba baadhi ya wajumbe
wametaka katiba ya jaji Joseph Sinde Warioba iwe ndiyo katiba itakayojadiliwa
huku wakitaka tume ya taifa ya uchaguzi kuwa huru ili kupata uchaguzi wa huru
na haki katika kipindi cha uchaguzi.
Kongamano hilo limeshirikisha wasomi
na wahitimu mbalimbali wa chuo kikuu cha Dar es Salaam ambapo mwenyekiti wa
kongamano hilo alikuwa ni Jaji Joseph Sinde Warioba.
Comments