AFISA MTENDAJI WILAYANI MPANDA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA
Na.Boniface Mpagape-Mpanda
TAASISI
ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Katavi, imemfikisha katika mahakama ya
wilaya ya Mpanda Afisa mtendaji wa mtaa
wa Kawajense akikabiliwa na shtaka la kushawishi na kupokea rushwa ya shilingi
elfu thelathini.
Taarifa
ya TAKUKURU Mkoa wa Katavi kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Kaimu mkuu
wa TAKUKURU Mkoani Katavi Bw. Christopher Nakua imesema kuwa afisa mtendaji
huyo Bi. Catherine Kipeta, mnamo Jumatatu ya tarehe 18 mwezi huu aliomba rushwa
ya shilingi elfu thelathini kutoka kwa mwananchi ili asimpeleke kwenye baraza
la kata kwa kosa la kufungua sehemu ya biashara,muda wa kufanya usafi.
Amesema
TAKUKURU Mkoa wa Katavi ilifanya uchunguzi wa awali na kuandaa mtego na
kumkamata mshtakiwa baada ya kupokea rushwa kutoka kwa mwananchi huyo.
Mshtakiwa
amefikishwa katika mahakama ya wilaya tarehe 19 mwezi huu na kusomewa mashtaka
mawili yanayomkabili ambayo ni kuomba rushwa ya shilingi elfu thelathini na kosa
la pili ni kupokea rushwa, kinyume na matakwa ya mwajiri wake na kifungu cha 15
(1) (a) cha sheria ya kuzuia na
kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.
TAKUKURU
mkoa wa Katavi inatoa wito kwa wananchi wote kujiepusha na vitendo vya rushwa
ambavyo husababisha kutopatikana kwa haki, kutowajibika kwa watumishi wa umma,
kwenda kinyume na maadili, kanuni na viapo vya utumishi, uvunjaji wa haki za
binadamu, wananchi kukosa imani na idara, taasisi, mashirika mbalimbali ya
serikali.
Aidha,Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani Katavi imesema kila mwananchi ana
wajibu wa kutoa taarifa ya vitendo vya rushwa katika ofisi hiyo iliyopo Mpanda
mjini, au kupitia simu ya bure namba 113.
Wananchi
wanapaswa kutetea haki, kuzuia rushwa kwani rushwa ni adui wa haki, na penye
sheria pana haki, penye haki pana amani, penye amani pana maendeleo.
Comments