WANAFUNZI 1137 WATOKOMEA KUSIKOJULIKANA,AFISA ELIMU KUTANGAZA MSAKO NYUMBA KWA NYUMBA.
Na.Issack Gerald-Nkasi.
WANAFUNZI
wapatao 1137 kati ya 2257 hawajaripoti
shule kuanza kidato cha kwanza mwaka huu katika Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa licha
ya serikali kutoa elimu bure.
Akizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio kwa njia ya mawasiliano ya simu Kaimu Afisa Elimu sekondari
Wilayani Nkasi Bw. Fortunatus Kaguo amesema kuwa,jumla ya wanafunzi 2257
walichaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi sasa
walioripoti shuleni ni wanafunzi 1120 pekee huku wengine1137 wakiwa hawajulikani
walipo.
Aidha
Afisa elimu huyo amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao shule na atakayekaidi
atachukuliwa hatua kali za sheria.
Amefafanua
kuwa wanamikakati ya kuanzisha oparesheni ya nyumba kwa nyumba ili kuwasaka wazazi
ambao hawajawapeleka watoto wao shule.
Hatua ya kukosekana
kwa wanafunzi hawa kunafuatia ikiwa ni
muda mfupi baada ya Seriklai kutangaza mpango mkakati wa elimu bure kwa
wanafunzi kuanzia Chekechea hadi sekondari kwa wanafunzi wa kidato cha nne.
Comments