KAMANDA WA POLISI RUKWA AZUNGUMZIA HALI YA USALAMA SIKUKUU ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA,ASEMA MATUKIO MAKUU MAWILI YALITIKISA MWAKA 2015
Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa limesema
kuwa,hakuna matukio matukio ya uharifu yaliyotokea katika kipindi chote cha
msimu wa sikukuu za kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016.
Ramani inayoonesha mahali Mkoa wa Rukwa unapopatikana pia maeneo yanayopakana na mkoa huo yanaonekana |
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa
Polisi Mkoani Rukwa SACP Jacob Mwaruanda
wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kwa nji aya simu,kuhusu Tathmini ya
hali ya usalama katika sikukuu za krismas Desemba 25 na mwaka mpya 2016.
Amesema kuwa tukio pekee lililotokea
msimu wa sikukuu ni linamhusisha mtu mmoja mtembea kwa mguu aliyekufa baada ya
kugongwa na pikipiki Mjini Sumbawanga.
Aidha Kamanda Mwaruanda amesema,matukio
makubwa yalitokea kwa mwaka 2015 ni pamoja na Mauaji ya mtoto mwenye ulemavu wa
ngozi Albino na kuchomwa vifaa vya kupigia kura pamoja na gari wakati wa
uchaguzi wa mwaka jana wa urais,ubunge na udiwani.
Katika matukio ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino Mkoani
Rukwa,ni pamoja na tukio la mwezi machi mwaka 2015 ambapo Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi albino
Baraka Cosmas (6) aliyekuwa akiishi na wazazi wake kijijini Kipeta, Bonde la
Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga alishambuliwa na kujeruhiwa vibaya kwa kukatwa
kiganja cha mkono wake wa kulia na watu wasiojulikana kisha kutokomea nacho
kusikojulikana.
Hata
hivyo Kamanda Mwaruanda amesema mashauri ya watuhumiwa wa ukatiri kwa mtoto
huyu mwenye albino yanaendelea mahakamani.
Wakati
huo huo wakazi wa Mkoa wa Rukwa,wametakiwa kushirikiana na Polisi kwa kuripoti
matukio ya uharifu kabla hayajasababisha madhara kwa watu.
Asante kwa kuendelea
kuwa namii,endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Comments