VIONGOZI MKOANI GEITA WATAKIWA KUTOWAONEA AIBU WAFANYABIASHARA WASIOFUATA KANUNI ZA USAFI ILI KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU
Na.Issack Gerald-Geita
Viongozi wa Mkoa wa Geita wametakiwa
wasiwaonee aibu kuwafungia wafanyabiashara wasiofuata kanuni za usafi wa
mazingira na hivyo kupelekea mlipuko wa kipindupindu.
Hayo yamesema na Waziri wa Afya,Maendeleo
ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kambi ya
wagonjwa ya kipindupindu iliyopo kwenye kituo cha afya Nyankumbuli mjini Geita.
Waziri Ummy alisema mlipuko wa kipindupindu upo hivyo kuwafumbia macho wale
ambao wanafanya biashara katika mazingira yasiyo safi na salama lazima watu hao
wafungiwe
“ Wanasiasa wenzangu inabidi mtuelewe
,hivi sasa kuna mlipuko wa ugonjwa wa
kipindupindu katika mikoa ishirini na moja na ni haki ya kuhakikisha afya za
wananchi zipo safi na salama hivyo tutaruhusu biashara zilizopo kwenye
mazingira safi na salama na endapo tutakua tumejiridhisha kwamba wafanyabiashara wamezingatia kanuni za usafi
wa mazingira”
Aidha, ameupongeza mkoa wa Geita kwa jitihada
za kudhibiti wagonjwa wapya kwa wiki hii kuliko wiki iliyopita ambapo kwa wiki
hii kuna wagonjwa wapya wanne,ukilinganisha na wagonjwa nane wa wiki iliyopita,hivyo ameutaka mkoa kuendelea kutoe elimu kwa
wananchi kuhusu ugonjwa huu.
Wakati huohuo waziri Ummy amewataka watumishi
wote wa kada za afya nchini kufanya kazi kwa mujibu wa maadili na kwa
kuzingatia viapo vya fani zao wakati wanapotoa huduma kwa wananchi
Ummy alisema serikali haitowaonea
aibu kuwachukulia hatua kali kwa kila
mtumishi atakayetoa lugha mbaya na kukiuka maadili ya kazi zao wakati wa kutoa
huduma kwa wananchi.
“Hatua kali tutachukua kwa yule
atakayebainika ametoa lugha isiyostahiki na inayomdhalilisha mgonjwa, hatutomvumilia kwakweli na hili
tutashirikiana na wenzetu wa Tamisemi kulifanyia kazi.
Awali, akisoma taarifa ya Mkoa wa
Geita kuhusu hali ya kipindupindu ,Mganga Mkuu wa mkoa Dkt. Joseph Kilasa
alisema Mgonjwa wa kwanza alipatikana mwezi wa tisa mwaka jana ambapo walipata mgonjwa wa kwanza toka mji wa katoro
ambaye alitokea jijini dare es salaam.Hadi sasa wamepata jumla ya wagonjwa 116
na watu saba 7 walipoteza maisha
Comments