SIKU YA PILI ZIARA YA WAZIRI MKUU, AKAGUA JENGO LA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGEA
Na.Issack Gerald-Ruvuma
Chanzo cha habari :Ofisi ya
mawasiliano ya Waziri Mkuu
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amekagua jengo la Makao Makuu ya Halmashauri ya Wialaya ya
Songea lilipo katika kijiji cha Lundusi, Wilaya ya Peramiho mkoani Ruvuma.
Makao makuu ya Halmashauri aya Wilaya ya Songea |
Alipowasili
jana katika eneo hilo alikutana na viongozi wa jadi ambapo Mzee
Daniel Gama alimkabidhi ngao na silaha ikiwa ni ishara ya
kumkaribisha kijijini hapo, pia alipata fursa ya kutazama ngoma ya mila ya
kabila la Wangoni.
Mara
baada ya kukagua jengo hilo la ghorofa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Lundusi Bwana Rajabu Mtiula amesema jengo hilo lenye ofisi 50, vyoo 4,
ukumbi mkubwa 1 na kumbi ndogo 2, ambapo mradi huo umetekelezwa kwa fedha za
mfuko wa Mradi wa Maendeleo na Serikali. Hadi sasa Serikali imetoa kiasi cha
zaidi ya shilingi bilioni 200 na utekelezaji wake umekamika kwa 85%,
hivyo wanatarajia kuanza kutumia jengo hilo mwezi Februari, 2016.
Akizungumza
jana na wananchi wa kijiji cha Lundusi, Waziri Mkuu, amewapongeza
wananchi wa Lundusi kwa hatua hiyo ya maendeleo na kusema kuwa
Serikali itaendelea kuunga mkono ujenzi wa jengo hilo.
Waziri
Mkuu Majaliwa, ametaka kuwepo na mikakati ya uboreshaji wa eneo hilo kwa
kusogeza huduma karibu ili kuvutia watu zaidi katika eneo hilo.
Naye,
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira na
Walemavu Jenista Mhagama ametoa pongezi kwa Mheshimiwa Rais Dkt.
John Magufuli na Waziri Mkuu kwa kuchaguliwa na kuongoza Serikali ya Awamu ya
Tano.
Pia,
ameishukuru Serikali kwa kusaidia kujenga jengo hilo, na pia ameeleza kero
mbalimbali zinazowakabili wananchi wa maeneo hayo ikiwemo wakulima kutofaidika
kwa bei ya soko ya kuuza mahindi, kutokuwepo na umeme na maji.
Aidha,
Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Waziri Jenista kufuatilia kero hizo kwa Wizara
husika na baadae kuleta mrejesho kwa wananchi.
Waziri
Mkuu Majaliwa ameendelea na ziara mkoani Ruvuma, leo siku ya jumanne ambapo
atatembelea na kukagua Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kuongea na Watumishi wa
hospitali hiyo na baadae ataongea na Watumishi wa Umma.
Asante kwa kuendelea kuwa namii,endelea
kuhabarika na P5 TANZANIA
Comments