HALMASHAURI ZA WILAYA KATAVI ZATAKIWA KUTATU CHANGAMOTO YA MIUNDOMBINU YA ELIMU KUFANIKISHA BRN
Na.Issack Gerald-MPANDA
HALMASHAURI
zote zilizomo ndani ya mkoa wa katavi zimetakiwa kufanya jitihada za
kutatua changamoto za miundombinu ya
elimu ili kuhakikisha wanafunzi wote wanasoma vizuri.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Bw.Said Mwapongo wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA ofisini kwake kwa njia ya simu.
Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Katavi Bw.Said Mwapongo wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA ofisini kwake kwa njia ya simu.
Amesema tayari ngazi ya mkoa imekutana na
ngazi za halmashauri lengo likiwa ni kuangalia utatuzi wa changamoto hizo kutokana na ongezeko la wanafunzi katika
sule mbalimbali.
Aidha Bw mwapongo
ameitaka jamii kuwapeleka watoto shule bila kisigizio chochote cha kutokuwa na sare ya shule na kuwa kwa mzazi au mlezi atakosa sare ya
shule ampeleke atapokelewa huku jitihada
za kutafuta sare zikiendelea kufanyika.
Mkoa wa Katavi unaundwa na Halmshauri
5 ambazo ni Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda,Halmshauri ya Manispaa ya
Mpanda,Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo,Halmshauri ya Wilaya ya Mlele na
Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe
Comments