TAARIFA KAMILI YA POLISI KUHUSU WATU KUFA MAJI KATAVI BAADA YA GARI KUSOMBWA NA MAJI HII HAPA,POLISI WASUBIRI MIILI IELEE NDIPO IOKOLEWE
Na.Issack Gerald- Katavi
Miili mitano ya watu walikufa baada
ya gari walilokuwa wakisafiria kusombwa na maji katika Mto Koga uliopo mpakani
mwa Mkoa wa Katavi na Tabora imepatikana huku miili mingine mitano ikiwa
hajajulikana ilipo.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amesema kuwa hadi sasa wanasubiri miili hiyo mitano ambayo
haijapatikana mpaka itakapoibuka na kuelea ndipo juhudi za uokozi zifanyike.
Katika tukio hilo,miongoni mwa ambao
hawajapatikana ni pamoja mama mmoja ambaye alikuwa na watoto wanne.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa tukio
hilo linahusisha gari aina ya Toyota Pick Up yenye namba za usajili T597 BTC.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo
Mussa Juma ambaye ndiye aliyekwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi
Inyonga wakati wakisaidia kuvusha gari
hilo kabla ya kusombwa na maji amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 12:00
jioni.
Hata hivyo Bw.Mussa amesema kuwa
mambo yanayotakiwa kufanyika katika eneo hilo ni ujenzi wa mnara wa
mawasiliano,ujenzi wa kituo cha polisi,uwekaji wa alama katika daraja hilo
ambalo limekatika kabisa na kujenga daraja ambalo maji hayawezi kupita juu yake
kama ilivyo sasa.
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa
kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ndiye Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk.
Ibrahimu Msengi ametoa agizo kwa viongozi wa usalama Mkoani Katavi kusitisha
safari za mabasi,gari ndogo na gari za mizigo
kutoka Mpanda-Tabora na Tabora-Mpanda kutokana na daraja la mto koga
kukatika na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watano.
Hili linakuwa tukio lingine la kusikitisha
katika historia ya Mkoani Katavi baada ya Basi la kampuni ya Sumry High Class
likiwa mtoni baada ya kupata ajali saa 7:30 usiku kuamkia Julai 5, 2013 katika
Mto Iku katika kijiji cha Sitalike wilayani Mlele mkoani Katavi ambapo maiti
tisa ziliopolewa katika ajali hiyo na majeruhi 53.
Comments