ASKARI POLISI KATAVI APIGWA RISASI YA TUMBONI AFA PAPOHAPO ENEO LA TUKIO- P5 TANZANIA INAKULETEA UNDANI ZAIDI
Na.Issack Gerald-Mpanda
Askari wa jeshi la polisi Mkoani Katavi
H305PC Nobert Stanslaus Chacha amekufa baada ya kupigwa risasi maeneo ya Kapanda
juu kata ya Machimboni Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amesema kuwa askari huyu amekufa baada ya kupigwa risasi ya tumboni
na risasi kutokea mgongoni.
Tukio hilo limetokea baada ya mkazi wa
Kapanda kuvamiwa na watu wasiojulikana ambapo baada ya mkazi huyo kufayatua risasi
ndipo ikampata askari huyo.
Kamanda amesema kuwa Mwili wa Marehemu Chacha umehifadhiwa katika chumba
cha maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda na jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.
Comments