TANZANIA YATANGAZA MIKAKATI ZAIDI UJENZI MIUNDOMBINU YA BARABARA KATAVI
Na.Issack Gerald-Dodoma
Serikali imesema kuwa inaendelea na
mikakati ya kuhakikisha inatenga fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi barabara
za Mkoa wa Katavi kwa kiwango cha lami kuunganisha na maeneo mengine jirani kwa
ajili ya kukuza uchumi mkoani Katavi.
Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa
Tanzania bungeni Mjini Dodoma Kassim Majaliwa wakati akijibu swali la Mbunge wa
Mpanda vijijini Mheshimiwa Suleiman Kakoso aliyetaka kujua mipango ya serikali
katika ujenzi wa miundombinu ya barabara Mkoani Katavi.
Juzi
Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani alisema
kuwa mwaka huu wa 2016 baadhi ya barabara Mkoani Katavi zikiwemo
zinazounganisha mkoa wa Rukwa na Katavi zitakuwa zimekamilika.
Naibu
waziri Ngonyani alisema ujenzi wa barabara ya Sumbawanga hadi Mpanda
umegawanyika katika sehemu nne, ambazo ni Sumbawanga kanazi kilometa 75,
Kanazi-Kibaoni Kilometa 76. 6, Kibaoni- Stalike kilometa 72 na Stalike-Mpanda
kilometa 36.
Comments