BIL.31 ZAPITISHWA NA BALAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA MWAKA WA FEDHA 2016/2017
Na.Lutakilwa Lutobeka-Mpanda
Jumla ya madiwani 20 katika
halimashauri ya wilaya ya Mpanda wamepitisha bajeti ya shilingi bilioni 31 ya
mwaka 2016/2017 iliyopendekezwa na halmashauri hiyo.
Hayo yamejiri baada ya kikao cha
kujadili bajeti ya halmashauri ambapo Afisa mipango wa halmashauri hiyo Bw.
Phosphors Nsuri amesema kuwa bajeti hiyo imezingatia dira ya maendeleo ya
halmashauri ikiwa pamoja na huduma za kijamii na miundombinu.
Aidha pamoja na kupitisha bajeti hiyo
madiwani wameiomba halmashauri kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao
ili kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kikao
hicho ambaye pia ndiye mwenyekiti wa Halmshauri hiyo Mheshimiwa Hamad Mapengo
amewataka madiwani kuwajibika ipasavyo katika kata zao kwa kusimamia miradi
iliyopo katika kata hizo.
Mbali na kikao hicho cha balaza la
madiwani kuhudhuriwa madiwani hao, pia kikao hicho kimehudhuriwa na watalaamu
mbalimbali kutoka katika halmashauri ya wilaya ya mpanda pamoja na wanasiasa mbalimbali.
Comments