MKUU WA WILAYA NKASI ATOA RAI KWA MADIWANI WILAYANI HUMO KUHAKIKISHA WANATATUA CHANGAMOTO YA MAPATO YA HALMASHAURI
Na.Issack Gerald-Nkasi.
MKUU
wa Wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa Idd Hassan Kimanta amewaasa madiwani wa Wilaya
hiyo kuhakikisha suala la kukuza mapato ya Halmashauri inakuwa ajenda ya kudumu
kwao.
Akizungumza
kwenye kaikao cha baraza la madiwani Mkuu huyo wa Wilaya amesema madiwani wengi
wakati wakiwasilisha taarifa zao za kwenye kata, kila mmoja ameeleza changamoto
kadhaa zilizopo kwenye kata yake na kutaka zitatuliwe na Halmashauri.
Bw.Kimanta
amesema suala la kukuza mapato halitawezekana
kama halmashauri haitakuwa na fedha za kutatua changamoto hizo.
Halikadhalika
Kimanta amewataka madiwani kushirikiana na wataalam wa Halmashauri ili kupata
suluhisho la kukuza mapato ya ndani ya Halmashauri na kuweza kutoa huduma
sahihi kwa wananchi wanaowawakilisha.
Katika
Wilaya ya Nkasi wamekuwa wakikumbwa na changamoto za kukosa masoko ya
mazao,matatizo ya kukosa miundombinu bora ya shule ikiwemo vyumba vya
madarasa,nyumba za walimu na changamoto nyingine za kimaisha.
Comments