SITA WAFA MAJI BAADA YA GARI KUSOMBWA NA MAJI KATAVI, ZAIDI YA WATANO BADO KUPATIKANA,MKUU WA MKOA APIGA MARUFUKU MAGARI KUSAFIRI KUPITA MTO KOGA
Na.Issack Gerald-Katavi
Watu wapatao 6 wameripotiwa kupoteza maisha katika daraja la
mto Koga lililopo mpakani mwa mikoa ya Katavi na Tabora, baada ya maji yaliyotokana
na mvua kufurika na kusababisha watu hao kusombwa na maji.
Akizungumza na P5
TANZANIA MEDIA Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahri Kidavashari alisema
watu hao waliosombwa na maji baadhi ya miili 6 hadi sasa haijaonekana ambapo kati
ya hao ni wanawake wawili na watoto wanne.
Kamanda Kidavashari amesema kuwa watu hao wamefikwa na umauti
baada ya gari aina ya Toyota Pick Up yenye namba za usajili T597 BTC, kusombwa
na maji wakati likijaribu kuvuka Mto Koga.
Kufurika maji kwa daraja la Mto Koga, kumesababisha kukatika
kwa mawasiliano ya barabara kati ya miji ya Mpanda mkoani Katavi na Sikonge
mkoani Tabora, na kusababisha kero kubwa kwa mamia ya abiria.
Miongoni mwa waathirika hao ni wanawake na watoto, wanaotumia
miundombinu kwa ajili ya kwenda kliniki na shuleni, wamelazimika kulala eneo la
mto huo kusubiri maji yapungue.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, ajali hiyo ilitokea juzi
saa 12 jioni baada ya gari hilo lililokuwa likitokea Tabora kwenda mjini Mpanda
kufika katika eneo hilo la Mto Koga na kukuta foleni ya magari yakisubiri
kuvuka.
Inadaiwa kuanzia juzi zaidi ya magari 100 yalikuwa yamekwama
huku idadi kubwa ya abiria wakikwama pia katika eneo hilo na kulazimika hadi
maji yapungue.
Hata hivyo majina ya walikufa katika
ajli hiyo hayajafahamika.
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Mussa
Juma ambaye ndiye aliyekwenda kutoa taarifa katika kituo cha Polisi Inyonga amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa
12:00 jioni.
Katika gari hilo lililozama lilikuwa
na watu 11 ambapo kati ya hao watano wamethibitishwa kufariki dunia huku Dreva
wa gari hilo akiokolewa.
Kufuatia hali hiyo, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
ambaye pia ndiye Mkuu wa mkoa wa Katavi Dk. Ibrahimu Msengi ametoa agizo kwa
viongozi wa usalama Mkoani Katavi kusitisha safari za mabasi,gari ndogo na gari
za mizigo kutoka Mpanda-Tabora na Tabora-Mpanda
kutokana na daraja la mto koga kukatika na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watano.
Endelea kuwa na P5 TANZANIA MEDIA kujua
zaidi idadi kamili ya waliofariki kutoka jeshi la polisi
Comments