AFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA TUHUMA ZA UHARIBIFU WA MALI NA KUTELEKEZA FAMILIA.
Na.Issack Gerald-MPANDA
Mtu
mmoja mkazi wa mtaa wa Kasimba manispaa ya Mpanda jana amefikishwa katika
mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuharibu mali na kutelekeza
familia.
Hakimu
wa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda Bw. David Mbembela amemtaja mshtakiwa kuwa
ni Juma Balison mwenye umri wa miaka 27, na kwamba alitenda kosa hilo tarehe 30
mwezi desemba mwaka 2015.
Amemtaja
mlalamikaji katika kesi hiyo kuwa ni Magreth Joseph, na inadaiwa kuwa mshtakiwa
aliharibu vyombo vya ndani ambavyo ni ndoo sita za plastiki na masufuria manne
kwa kuviponda ponda kwa nyundo.
Inadaiwa
pia kuwa mshtakiwa alikataa kutunza watoto aliozaa na mlalamikaji Bi. Magreth
Joseph. Hata hivyo, mshtakiwa Juma Balison amekana shtaka hilo na kesi hiyo
imeahirishwa na itatajwa tena tarehe 17 mwezi huu.
Comments