MABALAZA YA MADIWANI MPANDA KUANZA VIKAO VYAKE LEO
Na.Issack Gerald-Mpanda
Balaza la madiwani Manispaa ya Mpanda
leo linatarajia kuanza vikao vyake kujadili masuala mbalimbali yanayohusu
maendeleo ya wananchi.
Moja ya mambo yanayoifanya Mpanda kupewa Manispaa ya Mpanda |
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA,mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda Mheshimiwa
Willium Philipo Mbogo,amesema kuwa pamoja na kujadili masuala mbalimbali,pia
wanatarajia kuchagua kamati mbalimbali zitakazokuwa chini ya balaza la madiwani
kwa ajili ya kusimamia shughuliza maendeleo.
Manispaa ya Mpanda,ni manispaa ambayo
inakabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo miundombinu mibovu ya barabara
zinazotoka mjini kuelekea vijijini,Upungufu wa miundombinu ya elimu shuleni
kama madarasa,upungufu wa walimu,huduma duni za afya katika hospitali ya
Wilaya,Zahanati na vituo mbalimbali vya afya,ukosefu wa maji safi na salama
katika maeneo mbali,mbali ya mji ikiwemo mtaa wa Mpanda Hotel Kata ya Mpanda Hotel ulipo katikati ya
Manispaa.
Wakati Manispaa ikifanya kikao
chake,Wakati huo huo pia balaza la madiwani kwa upande wa Halmashauri ya Wilaya
ya Mpanda watakuwa na kikao kama hicho,
Aidha changamoto zilizopo katika
Halmashauri hiyo ni Miundombinu mibovu ya barabara hali inayopelekea wakulima
kushindwa kutoa mazao shambani kupeleka mjini,ukosefu wa huduma za afya kwa
baadhi ya maeneo.
Hata hivyo Halmashauri hii ni miongoni
mwa Halmashauri ambazo zimekuwa zikivuka lengo la makusanyao ya mapato ya ndani
hadi asiliamia 100 huku wakazi wa halmashauri hiyo wakiendelea kupinga kelele kwa changamoto
zinazowadhibiti.
Mshirikishe mwenzako asikose habari kemkem za Katavi na
Kwingineko kupitia P5 TANZANIA MEDIA.Endelea
kufuatilia kitakachojili katika mabalaza ya madiwani Katavi
Comments