WAZIRI MKUU MAJALIWA ASEMA TANZANIA ITAENDELEA KUSHIRIKIANA NA RWANDA
Na.Issack Gerald
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Rwanda
nchini, Eugene Kayihura. Ambapo amemuahidi kuwa Tanzania itaendelea
kushirikiana na Rwanda.
Akizungumza
na Balozi Kayihura jana jumatano ofisini kwake, Magogoni jijini Dar
es salaam, Waziri Mkuu amemshukuru Balozi huyo kwa kumtembelea na
ameahidi kuwa Serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano ulipo baina ya nchi
hizi mbili.
“Nia
yetu ni kushirikiana kwa pamoja kwa kuunganisha wafanyabiashara wetu, kwa
kutumia Bandari ya Dar es salaam na reli ya kati, ambayo tutajenga
kwa kiwango cha kisasa ‘standard gauge’ ili ziweze kubeba mizigo
mingi na kwenda mwendo wa kasi” alisema Waziri Mkuu.
Kwa
upande wake, Balozi wa Rwanda, Kayihura amesema
Tanzania na Rwanda ni nchi marafiki na zinafanyakazi wa pamoja, Rwanda iko
tayari kushirikiana na Tanzania kikanda na kimataifa.
“Tunatumia
Bandari ya Dar es salaam na Mombasa, tunashukuru kwa namna ambavyo mnaboresha
Bandari ya Dar es Salaam, kwani Rwanda inafaidika pia kwa vile mizigo yetu
mingi karibu asilimia 75 husafirishwa kupitia bandari hii” alisema
Balozi Kayihura.
Comments