WAWILI MANISPAA YA MAPANDA WAFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA WAKITHUMIWA KUIBA NAKUPORA MALI ZENYET THAMANI KARIBU MIL.2.
Na.Boniface
Mpagape-MPANDA
MKAZI
wa Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda, Bw. Reuben Remi amefikishwa katika
mahakama ya mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la kuvunja duka na kuiba
nguo zenye thamani ya shilingi milioni moja na laki nne na elfu arobaini.
Akisoma
shtaka hilo mahakamani hapo, Koplo Mtei wa jeshi la polisi Mpanda, ameiambia
mahakama kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo desemba 28 mwaka jana, ambapo
alivunja duka la Bi. Rosana Mwamicheta katika mtaa wa majengo mjini Mpanda.
Mbele
ya hakimu David Mbembela, mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo na kuiomba
mahakama iruhusu dhamana.
Akitoa
masharti ya dhamana, hakimu Mbembela amesema, mshtakiwa anatakiwa awe na
wadhamini wawili ambao watawasilisha vitambulisho mahakamani, na mmoja kati yao
akabidhi dhamana ya fedha taslimu shilingi laki saba na elfu ishirini na
mwingine ahadi ya kiasi hicho cha fedha.
Kesi
hiyo itatajwa tena January 27 mwezi huu
na itaanza kusikilizwa january 28, na Mshtakiwa amerudishwa rumande hadi masharti ya
dhamana yatakapokamilika.
Wakati huo huo,mkazi
wa Kigamboni kata ya shanwe katika manispaa ya Mpanda Fredrick Josephat (18)
amefikishwa katika mahakama ya Mwanzo mjini Mpanda akikabiliwa na shtaka la
kuvunja nyumba na kuiba vitu vya ndani vyenye thamani ya shilingi laki tano na
elfu sitini na saba.
Imeelezwa
mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alitenda kosa hilo tarehe 03 mwezi huu nyakati
za usiku, nyumbani kwa Bw. Didas Boniface ambapo baadhi ya vitu vilikutwa kwa
mshtakiwa.
Hata
hivyo, mshtakiwa Fredrick Josephat amekana kutenda kosa hilo.
Hakimu
David Mbembela amesema mshtakiwa ana haki ya dhamana au anaweza kujidhamini
mwenyewe kwa kutoa fedha nusu ya thamani ya vitu vilivyoibwa, au mdhamini awe
mtumishi wa serikali na atoe kitambulisho na ahadi ya kulipa fedha shilingi
laki tano na elfu sitini na saba.
Mshtakiwa
ameshindwa kutekeleza masharti hayo, na amerudishwa rumande hadi atakapokamilika
masharti hayo na Kesi hiyo itasikilizwa tena tarehe 20 mwezi huu.
Comments