WAKURUGENZI WAWILI WATUMBULIWA MAJIPU YUMO WA SULEIMANI LUKANGA WA MANISPAA YA MPANDA
Na.Mwandishi wetu-DAR
ES SALAAM
MKURUGENZI Mtendaji Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Suleiman
Lukanga,amesimamishwa kazi kwa tuhuma za kuridhia na kutekeleza uamuzi ulioisababishia serikali
hasara na upotevu wa fedha.
Waziri George Simbachawene |
Taarifa ya kusimamishwa kazi sambamba na Mkurugenzi Mtendaji Manispaa
ya Kigoma Bw.Boniface Nyambele imetangazwa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene katika mkutano na
waandishi wa habari baada ya tangazo kutolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Ofisi ya Rais Tamisemi Rebecca Kwandu.
Kwa upande wake Mkrugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda
Bw.Suleiman Lukanga anayekabiliwa na tuhuma za ununuzi hewa wa gari la kusomba
taka kwa Sh milioni 92.75 na ubadhirifu wa fedha za ujenzi wa skimu ya
umwagiliaji ya Kakese, Sh milioni 294.
Naye Mkurugenzi Boniface Nyambele wa manispaa ya Kigoma
anayekabiliwa na tuhuma za uuzaji wa nyumba za halmashauri bila kufuata sheria,
kanuni na taratibu zilizopo, zinazomtaka awe na kibali cha waziri mwenye
dhamana.
Nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda itakaimiwa
na Lauteri Kanoni ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Katavi huku nafasi ya Mkurugenzi Manispaa ya Kigoma ikikaimiwa na Sultan
Ndilowa ambaye ni Mkuu wa Idara ya Maji Manispaa ya Kigoma
Aidha,Waziri Simbachawene amewataka wakurugenzi watendaji wa
mamlaka za serikali za mitaa nchini kuwa makini katika kutekeleza majukumu yao
kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo.
Amesema serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu kwa
watumishi wote,ambao watakiuka matakwa ya sheria, kanuni na taratibu na
kutoweka mbele maslahi ya umma.
Comments